MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 9


 SEHEMU YA 09

TULIPOISHIA

Tuliendelea kupiga story pale mi na Meshack, ndani ya dakika thelathini Rayan aliingia pale ndani na mwanamke mzuri, mrembo zaidi yangu kama mara nane hivi, tulipoangaliana machoni wote tulishtuka, akaenda kuketi kwenye kiti mbali kabisa na sisi.


Kiukweli nilipata wivu na sikujua ule wivu unaletwa na nini


ENDELEA

Kila saa nilikuwa namgeukia naona tu wanaongea mambo yao lakini sikusikia kwa sababu walikuwa mbali kidogo na pale tulipokuwa sisi.


Baada ya kumaliza kula tuliondoka mimi na Meshack tukaelekea mpaka kwake, yeye alikuwa anaishi Msasani, sio mbali sana kutoka pale Masaki, nikalala pale mpaka asubuhi, kilichotokea huko katikati ya usiku we jiongeze tu maana yule alikuwa ni mpenzi wangu.


Asubuhi niliamka mapema kabisa, japo nilikuwa nimechoka lakini nilipaswa kwenda nyumbani nikabadili nguo halafu ndio niende kazini, Meshack akaniambia

“Mpenzi”


“Abee”


“We nenda nyumbani, jiandae uende kwa mama yako huko ulikosema kuna mzigo umepewa upeleke halafu utakuja kesho jumatatu kazini okay?”


“Nashukuru babe, basi mimi nikuache naona uber iko nje inanisubiri”


“Shika hii” alisema Meshack huku akinipatia hela ya matumizi


“Asante mpenzi” nilimbusu halafu nikaondoka zangu.


Nilipofika nyumbani nilijirusha tu kitandani nikapotea mazima, nikaja kushtuka saa saba mchana, yaani nimechoka mwili mzima, niko hoi bin taabani utadhani sijatoka usingizini.


Niliendelea kujilaza kwenye kitanda changu huku nikitazama darini nawaza mambo mengi, ghafla wazo la kumtafuta Rayan likanitokea.


Nilichukua simu yangu chap na kuamua kumpigia lakini hakupokea, ikabidi nimtumie ujumbe “Hello, mambo vipi?”


Rayan hakunijibu, bali alikuja kunipigia baada ya lisaa lizima, akaniambia “Hallo mrembo”


Nikasema “Uko powa wewe?”


Akanijibu “Niko poa sana lakini nimekumiss”


“Anhaa, mbona hukupokea simu?” nilimuuliza


“Ah nilikuwa masjid (msikitini) kidogo” aliniambia


“Mh unaswali?” nilimuuliza kwa mshangao kwani alikuwa hafananii mtu wa ibada kabisa


“Yeah kwani vipi unaniona muhuni ee?” aliniuliza


“Hamna sio hivyo, ila vijana wengi wa mjini kama wewe hawawezi kuswali”


“Hahaha….sio Rayan, mimi nitafanya uhuni wa aina yoyote lakini kamwe sitamsahau Mwenyezi Mungu”


“Hahaa…safi baba….anyway jana nilikuona mahali”


“Oh, Masaki sio?” aliniuliza


“Ndiooo”


“Okay hata mimi nilikuona, roho iliniuma sana Munnie, si unajua mi nakupenda” alisema


“Haaaah sasa kwa hiyo uliingia na mwanamke wako pale ili uniumize roho au?” niliuliza


“Hapana hapana, sio mwanamke wangu yule ni dada yangu….acha kunikosea heshima hivyo”


“Dada yako??” niliuliza


“Ndio, huniamini?”


“Sikuamini hata kidogo, mbona mzuri hivyo?” niliuliza


“Hahahaa sasa kama ni mzuri wewe kwani kisa mimi ni m’baya ndio ukajua dada yangu hawezi kuwa mzuri”


“Hahahaa hapana sijamaanisha kwamba wewe ni mbaya bhana” nilisema


“Bali?”


“Ah tuachane na hayo, I am sorry lakini kama jana nilikuudhi lakini unajua niko kwenye mahusiano ee”


“Najua, lakini moja ya vitu vinavyoniumiza akili, sijui ni akili gani nitatumia ili wewe uweze kuhamishia moyo wako kwangu”


“Rayan” nilimuita


“Naam”


“Hilo haliwezekani naomba tuwe tu marafiki please and please” nilimpa onyo


“Impossible, yaani kuliko nikupende halafu tuwe marafiki, ni bora tuwe maadui tusizoeane kabisa mimi na wewe, lielewe hilo, mi nakuwaje rafiki na mtu ninayempenda bana, unafikiri nitajisikiaje??” aliniuliza


“Khaa, wewe mwanaume, mimi nina mtu….but why unapenda ghafla sana, mimi hunijui, hujawahi kuniona before unasema unanipenda, hata mimi sikujui kabisa, na ninavyokuona khaa hata kama nisingekuwa kwenye mahusiano mimi nisingeweza kuwa na mwanaume kama wewe”


“Najua huwezi kwa sababu mimi ni mbaya sana Munira, lakini hivyo hivyo mimi nimekupenda, sina kitu, lakini naomba unielewe, na kama haiwezekani niambie leo leo ili nifute namba yako na nisikutafute tena” alisema


Nilifikiria kidogo nimjibu nini lakini kiukweli kwa mbaali nilimuona kama anakuja kuja, ila kila nilipokuwa nakumbuka maisha ambayo nilimkuta nayo kule kigamboni, basi nilijikuta nashindwa kumpenda na kujizuia kwa kasi maana mimi sitaki mwanaume ambaye hata kumuomba kitu naogopa maana najua maisha yake ni ya kuunga unga


Kitu kingine kilichokuwa kinanisumbua  ni suala zima la kuwa na mahusiano wakati nina mpenzi wangu ambaye ananipa kila kitu hapa duniani na anaonekana kuwa na malengo makubwa sana na mimi


“Munira” Rayan aliniita


“Abee”


“Wooow, unavyoitika mashaallaaah….” Alisema Rayan 


“Embu acha mambo yako, kwani nimeitikaje”


“Unaposema abee, mpaka viungo vyangu vimechangamka”


“Viungo gani?”


“Achana na hayo, nipe majibu basi, nijue swala yangu imekubalika au nimeswali bila malengo”


Nilivuta pumzi kisha nikamuambia Rayan “I am sorry mimi kiukweli wanawake wapo wengi watakupenda….lakini mimi sitaweza kuwa na wewe sitaki kuharibu malengo yangu, nimeshafika mbali please”


“Kwa hiyo mimi nitayavuruga malengo yako?” aliniuliza


“Sio hivyo ila please, huyu mwanaume ananipenda sana”


“Kwa hiyo nifute namba yako?” aliniuliza, nikasita kwanza, nilikuwa natamani tuwe hata marafiki lakini mara nyingi ukishamkatalia mtu basi huwa ni tiketi ya uadui mkubwa kati yenu.


Nikamuambia “Amua mwenyewe siwezi kukupangia Rayan, but please kwa hilo naomba unisamehe”


“Ok poa…bye” alisema


Sikuweza kumjibu, mpaka pale alipokata simu…………JE NI MWISHO WA KUTAFUTANA??

LABDA KUTAKUWA NA SEASON TWO

USIKOSE 


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI (10)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group