SEHEMU YA 10
Katika season one Mwandishi Mtaalam Mr AB, aliishia pale Munira alipokuwa amemkatalia penzi Rayan
Tujikumbushe kidogo
“Kwa hiyo nifute namba yako?” aliniuliza, nikasita kwanza, nilikuwa natamani tuwe hata marafiki lakini mara nyingi ukishamkatalia mtu basi huwa ni tiketi ya uadui mkubwa kati yenu.
Nikamuambia “Amua mwenyewe siwezi kukupangia Rayan, but please kwa hilo naomba unisamehe”
“Ok poa…bye” alisema
Sikuweza kumjibu, mpaka pale alipokata simu
TUENDELEE NA SEASON TWO SASA inayoandikwa na mwandishi Mr AB bado inasimuliwa na Munira Yassin
Baada ya kumkatalia penzi Rayan alininunia kabisa, hakuwahi kunitafuta na mimi vile vile sikuwahi kumtafuta kabisa.
Sasa baada ya kupita kama wiki mbili hivi, nilikuwa nimekaa nje ya ofisi mimi na mlinzi wa kike wa jengo la Ubungo Plaza, tukawa tunapiga story mbalimbali maana muda huo mimi sikuwa na kazi.
Yule mlinzi aitwaye Yasinta aliniuliza “Hivi yule kijana alikuja hapa siku ile ni mpenzi wako?” nikashtuka kidogo halafu nikamuuliza
“Kijana gani?”
“Kuna yule alikuja akiwa na gari zuriiii….na tattoo hivi” aliniambia nikajua anamuongelea Rayan
“Anhaa….we nawe mtu wa zamani kabisa unakumbuka?”
“Ndio, aliniuliza mimi kama upo….ndio nikamuita Kevin”
“Anhaa kumbe ni wewe…….ah yule bwana alikuwa ananitaka sema mimi nimemkataa si unajua niko na Meshack?” nilimuuliza
“Anhaa…nipe namba yake” aliniambia Yasinta nikashangaa
“namba yake tena? Ulimpenda au?”
“Hamna….ila napenda sana wanaume weusi wenye ndevu nyingi” aliniambia
“Hahaa…” nilicheka huku nikianza kuvuta picha Rayan alivyo, kweli ni kijana mzuri, mtanashati, anavaa anapendeza, na hata hivyo alikuwa anavutia mno, japo mimi nilijua maisha yake kwamba ni masikini wa kutupwa
“Nipe basi?” alisema yasinta
“Ah mimi namba yake sina nilishafuta, labda akinitafuta tena” nilisema kwa wivu tu ila namba ya Rayan nilikuwa nayo
“ooh jamani unamkataliaje kaka mzuri kama yule?” aliniuliza yasinta
“Ah mimi sipendi wanaume waliochora tattoo naonaga ni wahuni sana” nilisema
“Khaa….haya bana”
Basi baada ya maongezi mengi kuhusiana na Rayan, nilijikuta nashawishika kweli kuwasiliana naye, sio kwamba alikuwa hanivutii alikuwa ananivutia sana, alikuwa na swaga hata mbele ya watu ningepita naye basi ingekuwa ni sifa tosha.
Niliporudi nyumbani jioni, nilikuwa nawaza nimtext au nimuache nikawa nimeuzuia moyo wangu kumtafuta huku nikijidanganya kwamba kama kweli angekuwa ananipenda basi siku zote hizo lazima angekuwa ameshanitafuta mimi.
Muda wote sikuwahi kuihifadhi namba yake kwenye simu, ila ilikuwepo kwenye call history pamoja na kwenye upande wa SMS, nilipita kwenye SMS, nikaandika ujumbe “Hello” lakini kabla sijautuma roho ilisita na kujikuta ninaifuta.
Niliendelea kutamani kumtafuta, lakini kwa sababu mimi ni mwanamke sikutaka kujipendekeza, niliamini atanitafuta kama ananipenda
Kuna roho moja ilikuwa ikinishauri kwamba akinitafuta basi nimkubalie halafu nitakuwa nawachanganya na Meshack bila Meshack kujua.
Nikaihifadhi ile namba halafu nikaenda kwenye mtandao wa WhatsApp nikaangalie picha yake kwenye wasifu, lakini nilipofika nilikuta ameweka picha ya mikono yake tu iliyochorwa tattoo, huku akiwa amevalia saa na urembo urembo mwingine wa kiume kwenye mikono yake hiyo.
Nilimtazama kwa muda lakini sura yake sikufanikiwa, nikatoka WhatsApp na kuacha kumtafuta huku nikisema “Kwanza Yasinta amenikumbusha wa nini huyu?”
*
Siku mbili baadaye ilikuwa ni birthday yangu, sina hela halafu Meshack alikuwa anaumwa umwa, kwa hiyo sikuwa na ujanja kwenda kwenye birthday party yoyote
Nilikaa tu nyumbani maana ilikuwa siku ya jumapili ambayo ofisini huwa hatufungui, nikatafuta picha yangu nzuri kabisa, nimevaa wigi kama la Mange Kimambi halafu nikapost kwenye WhatsApp status na kuandika hivi
“Happy Birthday to me mtoto wa mama Yahya……asante Mungu kwa rehma zako bado ni mzima wa afya, ila miaka niliyofikisha sitaji”
Nilipomaliza kupost to hivi, akanipigia Meshack na kuniomba niende nyumbani kwake kuna kazi nikamsaidie saidie kwa sababu alikuwa anajisikia vibaya sana.
“Sawa nakuja baby” nilimjibu
“Ok sasa hivi please”
“Sawa”
Nilijiandaa kisha nikaondoka kuelekea Masaki alipokuwa akiishi mwanaume huyo, nilipofika Masaki nilimkuta akiwa nje ya nyumba anapunga upepo, nikamsalimia, tukaongea ongea halafu nikaanza kufanya usafi ndani na nje ya nyumba yake.
Nikiwa nafanya usafi chooni, nilisikia mlio wa simu yangu ikiita, nikatoka haraka na kuiwahi ilikuwa sebuleni, nilipoangalia nani anapiga, nikagundua ni Rayan
Nilishtuka na kujiuliza Rayan ananitafuta anataka nini tena?...........JE RAYAN ANATAKA NINI KWA MUNIRA?? USIKOSE SEHEMU YA 11
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)
