SEHEMU YA 11
TULIPOISHIA
Nikiwa nafanya usafi chooni, nilisikia mlio wa simu yangu ikiita, nikatoka haraka na kuiwahi ilikuwa sebuleni, nilipoangalia nani anapiga, nikagundua ni Rayan
Nilishtuka na kujiuliza Rayan ananitafuta anataka nini tena?...........
ENDELEA
Nikachungulia nje ili Meshack akawa ananisikia, nilipoona yuko mbali, nikapokea simu na kusema “Hallo”
“Hallo mambo?” aliniuliza
“Safi tu niambie”
“Happy birthday to you” alisema Rayan
“Mh, tena? Rayan umejuaje leo birthday yangu?”
“Ah kwani si umeweka status naona jamani?” aliniuliza
“Ahaa, asante kwa kuniwish”
“Ok, sawa ila nimekumiss pia” aliniambia
“Umenimiss?? Mbona hujanitafuta?”
“Sa kama uliniambia nisikutafute ningethubutu vipi?”
“Sasa leo umethubutu vipi?”
“Ah basi sorry kama nakuudhi bye” alisema
“no usikate simu kwanza” nilisema lakini Rayan alikata simu kwa hasira, alionekana hakufurahishwa na maswali yangu niliyokuwa nikimuuliza, ndipo nikamtumia ujumbe “Sorry, and thanks for wishing my birthday”
“Ok” alinijibu
Niliweka simu pale pale kisha nikaenda kuendelea na usafi, nilipomaliza nilipika tukala mimi na Meshack halafu tukawa tunaangalia muvi taratibu ndani huku tunaongea mambo ya biashara.
Saa moja usiku ndipo nilipomuaga naondoka kwenda kwangu, naye alikubali bila wasiwasi, sasa nikiwa njiani, kwenye foleni za Mwenge, nilipata mualiko kupitia SMS .
Mualiko ulisema hivi “Munnie, nakuomba Mlimani City, ninataka nisheherekee birthday yako kama haupo kwenye party leo” huu ulikuwa ujumbe kutoka kwa Rayan
“Saa hizi?” nilimuuliza
“Yes, ingependeza zaidi”
“Haaa, sijajiandaa”
“Ok jiandae uje, usiogope chochote”
“sawa nitakuambia” nilimjibu
Safari yangu iliendelea mpaka nilipofika nyumbani baada ya dakika thelathini, nilikaa kwenye sofa nikawa nawaza namna nitakavyoenda kuianza wiki mpya nipate pesa nyingi, nikiwa nawaza vile, nilipata simu kutoka kwa Rayan
“Munira vipi mbona sikuelewi nimeshaandaa kila kitu naomba uje”
“Jamaanii…mbona nilikuwa nishasahau, unajua gari yangu haina mafuta?” nilimuambia
“Huna baki yoyote? Mafuta utakuja kuyapata huku au nikuagizie bolt?”
“Ndio inafaa”
“Ok dakika kadhaa” alisema na kukata simu
Ilibidi niende nikaoge ili nijiandae akija anichukue tuondoke, sikujua hata ni kitu gani kinanisukuma kwenda kuonana na Rayan, nilihisi kuna kitu anacho na nilitamani kukijua zaidi maana nilikuwa nimeshamuona kama ana roho nzuri hivi
Kweli ndani ya dakika ishirini bolt hii hapa, nikaondoka naye kuelekea Mlimani city, nilipofika nilikuta Rayan na marafiki zake wameniandalia bonge la keki, pamepambwa, yaani kama masihara, halafu wananikaribisha kwa mbwembwe, huku wakisema “Shemeji, karibu uinjoy” mi nashangaa shemeji tena?.........ITAENDELEA
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12)
