MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 12


 SEHEMU YA 12

TULIPOISHIA


Ilibidi niende nikaoge ili nijiandae akija anichukue tuondoke, sikujua hata ni kitu gani kinanisukuma kwenda kuonana na Rayan, nilihisi kuna kitu anacho na nilitamani kukijua zaidi maana nilikuwa nimeshamuona kama ana roho nzuri hivi


Kweli ndani ya dakika ishirini bolt hii hapa, nikaondoka naye kuelekea Mlimani city, nilipofika nilikuta Rayan na marafiki zake wameniandalia bonge la keki, pamepambwa, yaani kama masihara, halafu wananikaribisha kwa mbwembwe, huku wakisema “Shemeji, karibu uinjoy” mi nashangaa shemeji tena?.........


ENDELEA

Nilishindwa kuwaambia kwamba mimi sio shemeji yao lakini nikamsitiri Rayan usijekuta amewatambia wenzake kwamba mimi ni mpenzi wake.


Tukakaa pale kama masihara sikutarajia kama ningesheherekea siku yangu ya kuzaliwa kwa mbwembwe vile, Rayan alikuwa amenifanyia surprise ya ajabu ambayo sikutarajia.


Nilipewa zawadi pale na marafiki zake, tukakata keki na kulishana mpaka saa sita usiku tukawa tunakunywa vinywaji


Rayan alinishika mkono na kunipeleka kwenye kiti cha mbali kabisa na pale walipokuwepo marafiki zake, tukaketi


“Rayan”


“Nambie bestie” alisema


“Umewaambia wenzako mimi ni shemeji yao? Shemeji yao tangu lini?”


“Hahahaa….kwa hiyo umemaind?” aliuliza Rayan


“Hapana lakini nilishakuambia hali halisi halafu kingine wanaweza waropoke mbele ya Meshack na unajua kabisa mimi na wewe sio wapenzi” nilisema


Rayan alinitazama tu bila kusema neno, mimi nikamuuliza “Kwanini umeamua haya maisha?” 


Akanipachika swali juu ya swali “Maisha yapi?”


“Unapoishi hapafanani na wewe, hata vitu unavyovifanya mtaani unakuwa na hela, marafiki zako wana hela, mnatembelea magari mazuri lakini nilipoingia ndani kwako kiukweli nilishangaa na naendelea kushangaa mpaka leo” nilisema


“Achana na hayo, mimi nikuambie tu kitu kimoja ninakupenda sana” alinichana


“Sawa, kwa hiyo nilichokuuliza hakina maana?”


“We achana nacho mimi nitakuambia siku nyingine kwanini naishi maisha haya”


“Mh…sawa…asante kwa party na surprise”


“Usijali” alisema


“Kwa hiyo sasa”


“Nakusikiliza”


“Mi nataka niende nyumbani si unajua kesho asubuhi natakiwa niwahi kazini?” nilimuuliza


“Oh yes, sawa, twende nikupeleke”


“Ok”


Rayan alienda kuwaaga wenzake, halafu tulitoka nje, akachukua gari nzuri, mimi sikujua ni ya nani kati ya wale marafiki zake, tukaondoka taratibu huku akiwa ameweka wimbo wa James Arthur uitwao Say you won’t let go, ni mzuri niliupenda, huku tunapiga story tunatembea taratibu kuelekea Goba.


Nilikuwa nikimuelekeza ninapoishi mpaka pale tulipofika getini.


“Ndio hapa?” aliniuliza


“Ndio ni hapa, kwa hiyo tutawasiliana basi” nilisema huku nikifungua mkanda kwa ajili ya kushuka


Rayan hakunijibu alibaki akinitazama tu, nikamuuliza “Vipi mbona unanitazama sana?”


Rayan hakuweza kuvumilia, alinivuta kwa nguvu nikamsogelea halafu akanishika siwezi kufurukuta maana alikuwa ni mwanaume wa mazoezi


“Nini Rayan lakini?” nilimuuliza


Rayan alikuwa mpole, hata hakunijibu zaidi ya kunishika na kuhakikisha ameugeuza uso wangu ukatazamana na wa kwake kwa ukaribu, haongei chochote lakini ndio alikuwa anausogeza mdomo wake taratib kukutanisha na wa kwangu…………ITAENDELEA


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA TATU (13)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group