SEHEMU YA 08
Nikajipa majibu “Deni la ofisini atakata kwenye mshahara, hapa nikamtoe kwanza mama mwenye nyumba halafu itakayobaki itanisaidia kwenye matumizi yangu binafsi”
Jioni saa kumi na mbili niliondoka ofisini kuelekea nyumbani, nilipofika nilimkabidhi hela ya kodi mama mwenye nyumba, ikiwa ni siku ishirini kabla ya kodi yangu kuisha.
Nikaingia ndani nikaoga, halafu nikajiandaa kwa ajili ya kwenda date pamoja na Meshack ambaye ni boss wangu
Baadaye kidogo mida ya saa moja na nusu niliagiza Uber, nia yangu ilikuwa ni kwenda nayo maana nilijua siku ile naweza nikalewa halafu nikashindwa kuendesha gari,
Uber ilinipeleka hadi Masaki, kuna hoteli yetu safi ambayo tulikuwa tukipenda kwenda wakati tumemissiana.
Tulipofika tuliagiza vinywaji pale tukawa tunakunywa na nyama za kutosha huku tukipiga story mbalimbali hasa hasa Meshack alichokuwa anata kukifanya ni mimi kunioa.
“Unataka tuoane lini?”
“Mwezi wa kumi na mbili nataka tuoane, nataka mwaka mpya niule nikiwa na mke wangu Munira ndani”
Nikamjibu “Usijali kuhusu hilo, ninakupenda sana Meshack wewe ndiye umenifanya nijione elimu yangu sikupoteza muda kusoma”
Tukiwa tunapiga story, simu yangu iliita kwenye pochi, nikaitoa haraka na kutazama ni Rayan ananipigia simu, nikaitazama nasita kupokea maana najua Rayan angeweza kunilete ishu za mapenzi, nikasema “Huyu naye msumbufu” huku nikibonyeza batani ambayo ilifanya simu iwe silent
“Pokea tu hamna shida” Meshack alisema
Nikapokea “Hello vipi?”
“Safi mbona hujanitafuta??” aliniuliza
“Nimetoka kidogo na mchumba wangu” nilimjibu straight forward
“Anhaa uko naye hata sasa hivi?”
“ndio niko naye hapa unataka kuongea naye?” nilimuuliza
“No no no….nyie kuleni bata mimi nipo tu” alisema Rayan
“Hahaha unamuogopa shemeji yako?” nilisema hivi makusudi maana sikutaka Meshack anihisi vibaya kabisa kwani ni mwanaume ambaye anajielewa na ana uwezo mkubwa wa kuendesha maisha ya mwanamke na ya kwake pia
“Hahaa…basi ukitoka utanicheki” aliniambia Rayan
“Sawa”
“Poa”
Rayan alikata simu na mimi nikaiweka kwenye pochi yangu halafu nikaendelea kula. Meshack akaniuliza “Ni nani huyo?”
Nikamjibu “Ni yule shemeji yangu, ambaye aliniambia nipeleke mzigo kwa mama”
“Sawa kabisa…mbona anakusumbua sana leo?” aliniuliza
“Ah, unajua alidhani nimeshapeleka ile pesa ndio maana”
“Ah, kumbe alitaka upeleke leo?”
“Ndio baby….but kesho nitatoka mapema basi nimuwahi mama si unajua Kibaha mbali?” nilisema
“Yes, basi hamna tatizo” alisema Meshack
Tuliendelea kupiga story pale mi na Meshack, ndani ya dakika thelathini Rayan aliingia pale ndani na mwanamke mzuri, mrembo zaidi yangu kama mara nane hivi, tulipoangaliana machoni wote tulishtuka, akaenda kuketi kwenye kiti mbali kabisa na sisi.
Kiukweli nilipata wivu na sikujua ule wivu unaletwa na nini…..ETI HUU WIVU UNAHISI NI WA NINI? USIKOSE SEHEMU YA 09
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TISA (9)
