MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 7


 SEHEMU YA 07

TULIPOISHIA

“Usisahau kunitoa blacklist…..” alisema “Halafu shika hii” alisema nikamgeukia nikamuona amechukua bahasha ya kaki ndogo iliyokuwa na kitu ndani akaniambia “Itakusaidia kupunguza deni lako hilo halafu tutawasiliana”


Nilirudi hatua mbili na kupokea ile bahasha, nilipochungulia ndani, kibunda cha noti za elfu kumi kumi hiki hapa….nilimshangaa kwanza, na sijui alileta za nini, nikamuuliza “Hizi za nini?”


“Tutawasiliana” alisema halafu akawasha gari akateleza


ENDELEA

Nilibaki naliangalia lile gari linayoyoma linapotea kule kwenye barabara, nikajisemea moyoni, hivi huyu kaka ananitaka nini mbona simuelewi elewi, au ametumwa nini, mara nikasikia sauti ya Kevin


“Sister husikii boss akikuita?”


Nikageuka haraka na kuanza kupiga hatua kuelekea ofisini “Ninakuja” nilisema huku nikiingia mlangoni na kuweka pesa kwenye droo yangu halafu nikamfuata boss pale ofisini kwake


“Boss samahani nilienda cho….” Kabla sijamaliza kudanganya akaniuliza 


“Huyo uliyekuwa unaongea naye hapo nje ni nani?”


“Ah…mh oh…ni mume wa dada yangu, amenipatia mzigo nimpelekee mama nyumbani” nilisema uongo


“Kwani yeye kashindwa kupeleka?”


“Ah…mh ndio boss, majukumu yamembana”


“Sawa....nilikuwa nakukumbusha lile faili la Jemedari William lichukue ufute deni maana jana alinitumia pesa yote”


“Sawa boss”


“Ok” alisema


Nilitoka kule ofisini kwake, nilikuwa na shauku ya kwenda kujua Rayan amenipa kiasi gani cha fedha nilipofika nilifunga mlango wa ofisi yangu halafu nikatoa pesa kwenye droo na kuanza kuzihesabu taratibu.


Kilikuwa ni kiasi cha shilingi laki tano cash, hakika sikuamini, ilibidi nijitikise tikise na kujifinya ili niamke maana nilikuwa nahisi ile ni ndoto tu.


Nilisema moyoni “Sasa kwanini ameniletea hizi pesa? Au ndiye aliyeniibia jana ndo amekuja kunipunguzia? Hamna huyu atakuwa ana pesa nyingi sana wale marafiki zake wanaonekana wana pesa za kutosha”


Nilitabasamu kwa furaha huku nikishika simu yangu na kuitoa namba yake kwenye blacklist halafu nikamtumia ujumbe


“Rayan” nilituma jina lake


“Naam, umeshanitoa kwenye blacklist?”


“Ndio, I am sorry zilikuwa ni hasira tu”


“Usijali, nahisi ulikuwa unadhani mimi nimehusika kwenye kuiba pesa zako, lakini kwa kifupi hapana”


“Sawa nimekuelewa” nilimuambia


“Ndio, sorry sijaweza kupata kiasi cha kukutosha, mimi sina hela, biashara yangu imedorora hapo nimekopa pesa kutoka kwa marafiki zangu watano tofauti ndio ikafika hiyo laki tano, usije ukadhania mimi nina pesa nyingi tuko tu mjini tunauza sura hivi, stress kibao”


“Usijali, unaonekana una roho nzuri, sikujua upo hivi tangu mwanzo, lakini vile vile Mungu akubariki na usiseme ni kidogo kwa sababu nisingeipata kokote kule”


“ok poa, pambana na kazi, ukitoka jioni naomba unicheki” aliniambia


“Sawa nitakucheki”


Nilikuwa nimefurahi sana kwa ule wema alionitendea Rayan, nilimuona mtu wa maana sana kwangu, nikashika tama na kuwaza mambo mengi, hususani lile deni la ofisi pamoja na pesa ya kodi ambayo nilikuwa natakiwa nilipe mwisho wa mwezi, shilingi laki tatu, maana chumba changu nilikuwa nikilipa shilingi laki moja kwa mwezi……………JE UNAHISI NINI KITATOKEA KATI YA HAWA WAWILI? USIKOSE SEHEMU YA 08


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA NANE (8)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group