MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 5



SEHEMU YA 05
“Hakuna shida, kwani kuna ubaya wowote wa kukupigia simu?”……

“Wewe sikiliza Rayan, mchezo mlionichezea leo, sio mzuri, unafikiri kwamba nitatetereka? Ninaomba mnikome tafadhali” niliongea kwa hasira maana nilijua ile shilingi milioni moja waliolipa pale kituo cha polisi, ndio wamenizunguka na kuniibia tena

“Mchezo gani tena?” aliniuliza kana kwamba hajui

“Usinifanye mi mtoto” nilisema kwa hasira halafu nikamsonya na kumkatia simu

Rayan hakukoma aliamua kunipigia simu kwa mara nyingine nikawa ninamkatia, mwishowe akanitumia ujumbe
“Samahani sana….mimi sijui kitu kilichotokea, lakini naomba uniambie uko wapi tuonane sasa hivi unieleze kilichotokea”

Yaani hasira zilinijaa, ananiganda ganda nini? Nikamkaushia lakini bado akatuma nyingine
“Unaishi wapi Mrembo? Unajua hata jina lako sijalijua?”

Nikamjibu “Rayan, usijizime data, wewe na wenzako mmenizunguka mkaja kuniibia zile pesa mlizolipa? Nakushauri kwamba usinizoee, nitakufunga”

Rayan akapiga tena, round hii nikapokea “Enhee” nilisema

“Unasema hela wamekuibia? Wamekuibia vipi? Mbona unanichanganya?” aliniuliza

“Kwa hiyo wewe unajifanya hujui?”

“Sijui kweli na sihusiki, vile vile washkaji zangu sidhani kama wanahusika katika tukio hilo”

“Haujui eenh?” niliuliza na nilijua anadanganya tu

“Kweli sijui, na pole sana kama limekutokea hilo, naamini umeyaona maisha yangu vizuri, ningekuwa nayo ningekusaidia hiyo pesa” aliniambia

“Embu kwenda zako usinitafute tena nitakublock mbwa wewe”

“Sawa” alinijibu

Rayan alikata simu, mi sikumuelewa kwanini alikuwa ananitafuta tafuta kila muda, wala sikuhangaika naye tena kwani nilikuwa nina stress halafu nilikuwa namuona kama mwanaume asiyejielewa, yaani mtu anapendeza barabarani lakini hana kitu kabisa.

Nilishuka kitandani, maana ilikuwa imeshafika mida ya saa moja jioni na nilikuwa na njaa ya hatari yaani.

Nikajishauri kimoyo moyo ‘hapa ninaenda kununua chips na mishkaki elfu nne halafu nanunua na juisi ya elfu moja nije nile nilale’

Hilo ndilo lilikuwa wazo langu la msingi, kweli nikavaa nguo zangu vizuri halafu nikatoka na kwenda mtaani kwa ajili ya kwenda kutafuta chips.

Nilipomaliza nilirudi ndani, nikawasha tv nikawa nakula huku naangalia taratibu.

Rayan hakuishia pale, aliendelea kunisumbua na message wakati nakula, aliniamua kunichana kabisa

“Oya, naomba nikuulize swali moja” lakini mimi sikumjibu akatuma nyingine “Nikuambie kitu bwana, mimi nimekupenda, ninahitaji uwe mpenzi wangu maana nimeona unanifaa kichizi”

Ilibidi nicheke kwanza, nilijiuliza yule mwanaume ambaye ana maisha magumu vile, ananifananisha? Ananiona mimi mjinga kama wasichana aliokuwa akiwatapeli mjini? Nikamblock kwanza ili ashike adabu halafu nikajisemea “Mtu huna zaidi ya nguo na kipande cha godoro halafu unasema eti nakufaa, wewe mbwa nini?” ITAENDELEA


Simulizi ya Kweli: MUNIRA AFISA MIKOPO


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA SITA (6)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group