MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 4

 



SEHEMU YA 04


TULIPOISHIA

Nilirudi kwenye gari yangu ili niendelee na safari, ile naangalia ndani ya gari, ile bahasha ya pesa haikuwepo ndani kabisa maana niliiweka kwenye siti ya mbele ambayo sio ya dereva.


Kiukweli nilichanganyikiwa


ENDELEA

Nilitafuta kwenye gari, hadi kwenye buti lakini sikuona kitu, nikaingia kwenye gari na kuanza kulia sana, milioni moja ni sawa na mshahara wangu mara tatu nab ado nitadaiwa laki. Niliumia kwa sababu sikujua nitamjibu nini boss.


Nililiondoa gari pale nilipokuwa nimepaki nikaendesha mpaka ubungo Plaza ambapo ndipo kulikuwa na ofisi zetu, sikushuka kwanza kwenye gari, nilikaa nikawaza kwa muda mrefu sana, ndipo nilimuona boss anatoka huku akiwa ameshika simu mkononi.


Alienda kuiegemea gari yake halafu akanipigia, simu yangu ikaita, mimi namuangalia tu sitaki kupokea nawaza nitamueleza nini, machozi yananilenga lenga namtazama tu.


Ghafla kama vile alihisi niko pale baada ya kuiona gari yangu, akajiegua kwenye gari yake halafu akaifuata gari yangu, na kusimama kwenye kioo akawa anachungulia.


Sijui halata alinionaje, akaanza kugonga kioo huku akisema “We nakupigia simu kumbe upo hapa na hupokei simu?” aliniuliza ikabidi nishushe kioo nikamtazama


“Boss” nilisema huku machozi yakinitoka


“Vipi Munira kuna tatizo?” aliniuliza mimi nikakaa kimya, akasema “Mbona kama unalia kimekutokea nini?”


Nilichukua leso yangu na kufuta machozi halafu nikamuambia “Wamenilipa milioni moja, lakini boss, wamenichezea mchezo wakaziiba” niliongea


“Unasemaje?”


“Ndio boss, nisamehe mimi sikujua”


Meshack alinitazama kisha akaniambia “Embu shuka kwenye gari uje tuongee ofisini”


Nikashuka kwenye gari halafu nikaenda ofisini na Meshack, akaniuliza “Umesema imekuwaje?”


“Boss, nimeenda kule Kigamboni, wamelipa hela, ni vijana wahuni wenye matattoo mwili mzima, walipolipa mimi niliondoka kwenda kupanda gari yangu posta, nilipokuwa nakuja kuna pikipiki iligonga gari yangu kwa nyuma”


“Enhee”


“Ikabidi nishuke nikaangalie kama gari imeharibika, nilipofika kuangalia, nikakuta imetoka rangi kidogo, nikarudi ndani ya gari hakuna bahasha yenye pesa wameshazichukua”


“Munira…..wewe una upumbavu mwingi sana” alisema Meshack kwa hasira ikabidi nipige magoti


“Nisamehe boss, utanikata kwenye mshahara wangu hamna shida” nilisema


“Haya usipige magoti inuka sasa, ndio maana mimi sipendi kufanya biashara na vijana bila kuwajua kiundani, yaani wengi ni matapeli sana” alisema Meshack


“Nisamehe boss, ni umakini wangu”


“Ok, basi tutaangalia utaratibu tutakaofanya maana hapa tutakuwa tumepata hasara kubwa sana”


“Sawa”


Meshack alikuwa ni boss wangu lakini vile vile alikuwa ni mpenzi wangu, hivyo hakuweza kunifokea sana, kichwani nilijua mshahara wangu utakuwa unakatwa nusu kwa nusu mpaka deni litakapokamilika maana pesa ilikuwa imepotelea mikononi mwangu, nilipata stress kwa sababu nilikuwa ninatakiwa nilipe kodi mwezi uliokuwa unafuata.


Baadaye baadaye Meshack aliniambia “Naona hauko sawa, utakuja kukosea tena mahesabu, naomba uende nyumbani ukapumzike mpaka kesho”


“Sawa nashukuru sana”


“Ok”


Nilitoka nikapanda gari na kuondoka kuelekea nyumbani ambapo nilikuwa naishi Goba.


Nilipofika nilioga, nikajiegesha kitandani, nikapotelea kwenye usingizi mzito sana.


Baadaye nilikuja kushtuliwa na simu yangu iliyokuwa inaita, nilipotazama ni namba mpya, nikapokea na kusikilizia sauti.


Nikasikia “Hallo” sauti ya mwanaume ilitoka upande wa pili


“Hallo za saa hizi?” nilisema


“Safi, uko wapi?” aliniuliza


“Wewe nani?”


“Mimi Rayan Kazimoto, uliyenifuata kigamboni” aliniambia


“Haaa….Rayan?” niliuliza kwa mshangao


“Ndio, mbona kama umeshtuka?”


“Hamna, kwani kuna shida gani hadi unanitafuta?”

JE KWA NINI RAYANN KAMTAFUTA MUNIRA


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TANO (5)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group