SEHEMU YA 03
TULIPOISHIA
Nilipatwa na hasira “Mpumbavu wewe…usiniambie ujinga hata siku moja” nilisema ila akanishika bega na kunizungusha “Unafanya nini?”
“Haah huku nyuma mashallah” alisema ndio kabisaa, hasira zikanijaa nikaupiga mkono wake uliokuwa umenishika halafu nikamzaba kibao cha maana shavuni
“Mpumbavu wewe” niliongea kwa hasira “Afande njoo…mkamate huyu mpuuzi” nilisema huku nikiufungua mlango ili afande aingie
ENDELEA
“Vipi kuna tatizo”
“Mfunge pingu mshenzi huyu, mimi ninakuja kwa ajili ya madeni yeye ananiletea tabia zake za kipumbavu” niliongea
Askari alimtazama Rayan kwa hasira, akamsogelea na kumuuliza “Unamtania afisa mikopo??” halafu akaanza kumpigia
Rayan alifungwa pingu tukatoka naye mpaka kituo cha polisi kwa mwendo wa taratibu, tulipofika kituoni pale aliwekwa sero, mimi na Kevin tuliondoka tukaendelee na majukumu mengine ya kila siku.
*
Kesho yake saa nne asubuhi nilipokea simu kutoka kwa yule askari, akaniambia nijitahidi nifike kituoni pale muda ule ule kwani kuna watu walikuwa wamefika kwa ajili ya kumuwekea Rayan mdhamana, nikaenda mpaka kituoni, nilipofika nilikutana na njemba tatu za nguvu, zinakuja kwa vitisho, kila mmoja ana gari yake vijana hasa, wote wana tattoo, wawili wakiwa na bleach kichwani huku mmoja akiwa na rasta.
“Hey madam” aliniita yule mmoja mwenye Rasta
“Vipi?” niliuliza
“Wewe ndio umemkamata mwanetu?”
Nilimtazama yule kijana, nikawaza mara mbili tatu nisije nikapigwa pale pale kituoni maana walikuwa wanaonekana wakorofi na midomoni walikuwa wakitafuna big G. “Kijana yupi?” niliuliza
“Rayan”
“Ahaaa nyie ndio mnamuwekea mdhamana?”
“Ndio….kwani anadaiwa shilingi ngapi?”
“Laki saba ya kampuni, na hela ya usumbufu laki tatu”
“Anhaa, hahahaa” alinicheka kwanza “Yaani hiyo hela kidogo tu ndio inawapa kiwewe?” aliniuliza
Nikamuuliza “Kama ni kidogo kwanini alikuja kukopa? Si mngemsaidia hiyo hela nyie?”
Yule kijana alinitazama tu bila kujibu.
Baadaye tulienda kuongea na askari, wale vijana wakasema, hakuna haja ya kupelekana juu zaidi, inabidi walipe tu hiyo pesa.
Kweli nikapewa pesa, ikahesabiwa pale, halafu Rayan akaachiliwa na kila mtu akafuta njia yake.
Mimi nilienda na bodaboda mpaka kwenye pantone, ili nielekee posta nikapande gari yangu nirudi ofisini Ubungo.
Nikachukua gari yangu na safari ikaanza rasmi kuelekea Ubungo, nikiwa njiani kuna mtu alisimamisha gari kwa ishara, alikuwa ni binti mdogo tu mwanafunzi wa shule, nikajua anavuka barabara hivyo nikapunguza mwendo halafu nikamuonyesha kwa ishara apite.
Ghafla nikasikia gari yangu imegongwa kwa nyuma na pikipiki, nilishtuka na kuangalia ni nini kimetokea, nikakuta mwenye pikipiki ndio anajiokota aridhini, nilighadhibika halafu nikasogea mbele na kupaki gari pembeni nikashuka ili niangalie kile kilichotokea nyuma ya gari
Nilipoenda kutazama hivi, niligundua kuna mchubuko mdogo tu kwenye mlango wa buti, na yule mwenye pikipiki akanitazama kwa huruma
“Samahani dada yangu”
Nikamtazama kwa huruma halafu nikasonya “Msssssiiiieeew uwe makini sio kutuletea hasara zisizo na maana”
“Sawa sister” alisema huku akivuta mafuta na ile pikipiki ikaondoka.
Nilirudi kwenye gari yangu ili niendelee na safari, ile naangalia ndani ya gari, ile bahasha ya pesa haikuwepo ndani kabisa maana niliiweka kwenye siti ya mbele ambayo sio ya dereva.
Kiukweli nilichanganyikiwa…….JE BAHASHA YA PESA IMEENDA WAPI? USIKOSE SEHEMU YA 04
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA NNE (4)
