SEHEMU YA 02
Tukaulizia pale tukaonyeshwa chumba alichokuwa akiishi, tukaingia ndani ya korido na kugonga mlango
“Hodii”
“Nani?” sauti ilisikika ndani
“Sisi wageni wako” niliongea
Rayan alifungua mlango na kutoka akarudishia, aliponiona pale mimi na askari alishtuka sana, akasema “Duuh mbona polisi tena?’
“Nimekuja naye kukukamata, naomba tuongozane” alisema “La sivyo tuchukue vitu vyote vyenye thamani ya deni unalodaiwa na kampuni LPF” alisema
“Daaah jamani….basi tutoke nje” alisema huku akitoka nje ya nyumban na sisi tukamfuata mpaka nje ambapo tulimkuta Kevin akiwa anatusibiri pale na pikipiki
“Enhee….jana kwanini nakupigia simu unani-blacklist?” niliuliza
“Samahani, maisha magumu sana” alisema ikabidi nimkague kuanzia juu mpaka chini. Anaonekana kabisa mtu mwenye maisha mazuri, ni mwanaume ambaye alikuwa na na sura yenye mvuto sana, ndevu za kutosha, halafu zilikatwa kiufundi, mikononi alikuwa na tattoo zilizoandikwa mambo mbalimbali, halafu alivaa pensi na sendo za ngozi zilizoonyesha kuwa za bei ghali sana.
Nikamuuliza “Wewe unasema una maisha magumu? Maisha magumu unaonekana kabisa una maisha mazuri ila jeuri tu kwa sababu ulishapata pesa ya matumizi yako sio?”
“Sio hivyo, ila I promise, nitaleta wiki hii, biashara imekuwa ngumu hata duka nitalifunga muda si mrefu twendeni mkalione” alisema
“Stop that nosense, sisi dukani tumeshapita, tunachotaka ni pesa, la sivyo tunachukua kila ulicho nacho hapa nyumbani kwako” nilisema kwa hasira
“Sister hakuna kitu nilicho nacho ambacho kinaweza kufidia hiyo laki saba, cha muhimu labda mnikamate”
“Unaleta jeuri ee? Basi naomba tuingie chumbani kwako” nilisema
“Twendeni”
“Ok”
Tuliongozana mimi, yule askari pamoja na Rayan tukaingia ndani, tulipofika ndani, tulishangaa wote, kwa sababu sikutarajia kijana kama yule angeweza kuishi sehemu kama ile.
Ndani kulikuwa hakuna kitu, kulikuwa na Godoro jembamba limetandikwa chini, kilikuwa na viatu jozi mbili, aina ya Air force pamoja na nguo alizotundika kwenye misumari nyuma ya mlango
Nikamtazama, halafu nikakitazama chumba nikamuuliza
“Unaishi hapa wewe Rayan??”
“Ndio, kwani vipi”
Nilitikisa kichwa nikasema “Impossible, you cannot leave in this room, acha kututania bwana” nilisema
“Haya sawa basi nikamateni, navyowaambia uchumi umenishuka mnielewe jamani, nitalipa mwishoni mwa mwezi huu” aliniambia.
Askari akanitazama, macho yake yakaniuliza ‘nimfunge pingu au nimuache’
Na mimi macho yangu yakamjibu ‘subiri kwanza’ halafu nikamgeukia Rayan nikamtazama usoni kwanza, hafananii kuishi maisha ya kimasikini vile, na nilivyomuona nilijua ni mtu mwenye dili kubwa sana mjini, hapo ndio nikaamini ni tapeli, nikajua hata wadada naamini wakijigonga basi huwa anawadanganya tu,
Nikiwa nawaza tuchukue hatua gani, ndipo akanipigia boss nikapokea “Mmempata?” aliniuliza
“Ndio….tuko naye hapa”
“Mkamateni haraka” alisema kwa hasira
“Sawa boss”
Boss akakata simu kisha nikamuambia Rayan “Tunaondoka wote mpaka kituo cha polisi”
Akanijibu “Sawa, lakini naomba kuongea na wewe kitu kimoja, askari akiwa nje”
“Kwanini awe nje?” niliuliza
“Naomba please akae hapo mlangoni, halafu tutaongea siweza kufanya chochote”
Nikamtazama askari, akatoka nje na kunisubiri mlangoni pale.
Rayan alisogea na kuurudishia mlango halafu akanisogelea na kuniambia kwa sauti hafifu
“Oh My God…..you’re so beautiful” alisema
“Rayan, kuwa serious, hilo ndilo ulilotaka kuongea na mimi?”
“Ndio, najua mtanikamata nitaenda kituoni, lakini sikiliza hakuna kitu napenda kama mwanamke mwenye mwanya au mwenye dimpo, halafu cha kushangaza wewe una vyote hivyo”
Nilipatwa na hasira “Mpumbavu wewe…usiniambie ujinga hata siku moja” nilisema ila akanishika bega na kunizungusha “Unafanya nini?”
“Haah huku nyuma mashallah” alisema ndio kabisaa, hasira zikanijaa nikaupiga mkono wake uliokuwa umenishika halafu nikamzaba kibao cha maana shavuni
“Mpumbavu wewe” niliongea kwa hasira “Afande njoo…mkamate huyu mpuuzi” nilisema huku nikiufungua mlango ili afande aingie
HIVI HUYU RAYAN ANA AKILI KWELI? USIKOSE SEHEMU YA 03
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TATU (3)
