SEHEMU YA 15
Kwenye mida ya saa nne asubuhi Rayan alifika pale nyumbani na gari tofauti na ile ambayo nilimuona nayo mara ya kwanza na pia ni tofauti na ile ambayo alikuwa amenileta nayo nyumbani mara ya mwisho, yaani kil siku gari jipya tu
Tuliondoka haoo mpaka kigamboni, alikuwa anajua short cut mwanaume yule akanikatiza katika mitaa ya kigamboni, siwezi kuitaja hapa maana watu wanaweza wamtafute kaka wa watu.
Tulipofika mtaani kwao aliniambia “Kuna kitu ninataka nikakuonyeshe”
“Kitu gani?” nilimuuliza
“Twende nikakuonyeshe naamini utafurahia”
“Mh, we mwanaume sijui una nini? Sikuwa na utaratibu wa kuja huku hivi….yani sijui umenishawishi vipi”
“Munira nilishakuambia, huenda mimi ndiye mume wako ambaye nimeletwa kwako kwa njia ya kukopa kwenye kampuni yenu, siwezi kuhitaji uwe mbali, kuanzia umbo, sauti, dimple na mwanya wako siwezi nikakubali vikanichoropoka” alisema
“Hivi Rayan, kwanini unanipenda?” nilimuuliza
“Nakupenda kwa sababu ya hizo sifa nilizozitaja, naomba unielewe…..”
“Mimi nina mchumba siwezi kukubali kuwa na wanaume wawili” nilimuambia
Rayan aliniangalia sana machoni, halafu akageukia mbele na kuwasha gari tukaanza kuondoka kuelekea huko alikokuwa anataka twende tulienda mpaka kwenye mtaa mmoja, upo ndani ya mji, kumejengwa nyumba moja kali ndani ya fensi, akapiga honi, geti likafunguliwa.
Lilipofunguliwa tu tukazama ndani kweli ni pazuri, nyumba kubwa, mpya kabisa, iliyo na kila sifa ya nyumba bora ambazo kila mtu anatamani kuishi.
Tulishuka kwenye gari, naangalia pale ndani ya geti kuna parking ya magari yamepaki matatu yote ni mazuri halafu mawili kati ya yale yaliyokuwa pale, ndio yale aliyonifuata nayo kazini, na kunipeleka nyumbani siku kadhaa zilizopita, mi najiuliza ni wapi amenipeleka lakini sikuwa na namna zaidi ya kumsikiliza anieleze.
“Karibu” alisema huku akisogea mlango na kupiga viatu chini ili kuondoa mchanga asije akaingia nao ndani
“Asante” alisema
Tuliingia ndani ya nyumba sebuleni, kulikuwa kuzuri, sebule kubwa, juu ukutani kumepambwa na picha kubwa za Rayan na zingine ni watu wengine ambao sikuwahi kuwaona.
Kuna kila kitu ambacho binadamu timamu anapenda kuwa nacho sebuleni kwake. Akaniambia
“Karibu sana”
“Asante, hapa ndipo Aya Sophia?” nilimuuliza makusudi ili anidodose ni wapi pale
“Hahah…hamna hapa ni nyumbani tu, naishi mimi na huyo kijana wangu aliyefungua geti nje”
“Anhaa…..mbona sijaelewa, kwako kwani kule tulipofika siku ile ni wapi?”
“Hahaa….kule ni kwa kuzugia tu sipendi watu wanisome, wabongo wana roho mbaya sana” aliniambia
“Ni kweli, kwa hiyo hii nyumba ni ya wazazi wako au?”
“Hapana, ni moja kati ya nyumba zangu nilizo nazo hapa kigamboni, nikishirikiana na Dalali mwanamke, huwa nina real estate za kutosha” alisema
“Khaaa” nilishangaa kwanza, kumbe yule jamaa alikuwa na mali nyingi…………..ITAENDELEA
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA SITA (16)
