MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 16


 SEHEMU YA 16

TULIPOISHIA

 “Ni kweli, kwa hiyo hii nyumba ni ya wazazi wako au?” 


“Hapana, ni moja kati ya nyumba zangu nilizo nazo hapa kigamboni, nikishirikiana na Dalali mwanamke, huwa nina real estate za kutosha” alisema


“Khaaa” nilishangaa kwanza, kumbe yule jamaa alikuwa na mali nyingi


ENDELEA

“Vipi mbona unashangaa?”


“Unanidanganya Rayan” nilisema


“Sikudanganyi Muni, nilitaka kukuficha kwamba mimi ni masikini ili unipende kama nilivyo, lakini kiukweli nashindwa kuvumilia” aliniambia


“Mh, kwani unahisi ukinionyesha mali zako ndio utanichanganya?” nilimuuliza


“Sijamaanisha hivyo” alisema Rayan halafu akapiga magoti karibu yangu huku akinishika kidogo mapajani “Naomba unielewe, ninakupenda, niko tayari kukupa kila kitu, nina mali nyingi sana, ninahitaji wewe uache kazi tuanze kuishi wote mimi nitakufungulia biashara” aliniambia Rayan


“Mh hivi Rayan”


“Naomba usiniambie umekataa, ninakuhitaji, I promise nitakuoa hata wiki ijayo ukitaka”


Nilimtazama sana Rayan, uso wake ulionyesha kumaanisha, akasimama, na mimi akanisimamisha halafu akanikumbatia kwa nguvu sana huku akionge maneno yenye maana kubwa ya mapenzi, karibu na sikio langu.


Rayan hakuwa haba, alikuwa anajua kumbembeleza mwanamke sio siri, alinivuta vizuri halafu akaanza kuninyonya ulimi kwa mara ya pili.


Ulimi wake ni mtamu kama sukari, nilikuwa nalegea kila nilipokuwa nausikia ukigusana na wa kwangu,.


Ghafla simu yangu iliita kwenye pochi, Rayan akaniachia na kuniambia “Bila shaka simu yako ndio inayoita” 


“Ndio” nilisema huku nikiitoa kwenye pochi na kutazama ni Meshack ananipigia simu. Ilibidi nimgeukie Rayan kwanza


“Vipi?” Rayan aliniuliza


“Ah ananipigia”


“Nani mchumba wako au?”


“Ndio….ngoja nipokee”


“Sawa”


Nilipokea simu “Hallo Babe” nilisema


“Yes, uko poa mke wangu?” aliniuliza


“Niko poa, vipi wewe unaendeleaje?”


“Niko safi, uko wapi?” aliniuliza nikashtuka kwanza kwanini ananiuliza hivyo, 


Nikawaza haraka haraka asije akasema nimtembelee, au aseme anataka kuja nyumbani, nikamuambia “Niko kwa dada yangu huku Kinyerezi” 


“Anhaa, daah, nilijua upo nyumbani uje uchukue ile hela ya kodi uliosema” aliniambia


“Hapana baby, labda baadaye nikitoka huku”


“Saa ngapi?”


“Kwenye mida ya saa kumi”


“Ok sawa, si utakuja kulala?”


“Hamna shida”


“Ok”


Meshack alikata simu, alikuwa hana mambo mengi sana, alikuwa hapendi kunichunguza wala kunifuatilia kama walivyo watu wengi kwenye mahusiano.


Nilimtazama Rayan akaniuliza “Vipi mbona kama umeshtuka?”


Nikavuta pumzi kisha nikasema “Hamna, alikuwa anataka nikamuone”


“Okay kwa hiyo unaenda?”


“Hapana nimemuambia nitaenda baadaye”


“Sawa, twenzetu, tukainjoy kidogo Aya Sophia halafu tukimaliza utaenda huko”


“Sawa”


Tulitoka pale ndani kwa Rayan tukapanda gari na kuondoka kuelekea kwenye hoteli hiyo ya kifahari, tulipofika kulikuwa na vivutio vya aina nyingi sana.


Tuliinjoy, tulipiga picha nyingi, tulikula vizuri sasa ilipofika mida ya saa nane tukaanza kunywa, mimi siku ile nilikuwa savanna, yaani kitendo cha kunywa savanna zote zilihamia chini.


Nikapandwa na hamu ya kufa mtu, namtazama hivi Rayan, ninashindwa kummaliza, kwa sababu pia ni mtu ambaye nilikuwa na hisia naye, nikamuambia “Rayan twende kwako tuka….mbane” niliropoka kweli kweli


Rayan akalipia fasta hakutaka kupoteza bahati, tukapanda gari yake na kuondoka kurejea kwenye ile nyumba aliyokuwa ameniambia ni ya kwake.


Tulipofika hivi, tuliingia moja kwa moja chumbani, tukakumbatiana….weeee kilichonikutaaaa……….ITAENDELEAAAA


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA SABA (17)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group