MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 14


SEHEMU YA 14

Ilikuwa ni siku ya jumatano jioni, nilikuwa nimetoka kuoga mara tu baada ya kutoka kazini, nikakaa mwenyewe nina furaha kwa sababu kesho yake sikuwa naenda kazini kwani ilikuwa ni sikukuu.


Hata hivyo nilikumbuka kwamba nina miadi ya kuonana na Rayan siku inayofuata ambayo ilikuwa alhamis ya Mapunduzi ya Zanzibar.

Nilichukua simu nikiampigia

“Hallooooo Rayan” nilisema


“Hallo mambow”


“Poa uko wapi mbona kama kuna kelele?” nilimuuliza


“Niko nacheki boli hapa”


“Leo timu gani?”


“Ah mipira hata sielewi naangalia tu baada ya kukosa cha kufanya, tena at least umenipigia ngoja nitoke hapa tuongee au uko bize?”


“Hapana tunaweza kuongea”


“Ok powa ngoja nitoke halafu nitakupigia sawa?”


“Sawa”


Nilikata simu, kiukweli nilikuwa nishakuwa na ile hamu ya kuwa nawasiliana naye kila muda lakini nilikuwa najizuia kwa sababu sikutaka nimpende, kijana yule niliona hanifai kuwa mume wangu kwa sababu mimi napenda magentlemen ambao hawana utoto, kwa hiyo yule niliona bado ujana ni mwingi hata ukiangalia maisha aliyokuwa anayapenda ni maisha ambayo sio ya mtu kumiliki familia.


Ilipita kama robo saa ndipo alinipigia simu nikapokea akaniita “Munira”


“Abee” nilisema


“Woow, unaitika vizuri hadi ninachanganyikiwa jamani”


“Nimeitikaje jamani?”


“Sijui hata nisemeje, umeitika kama vile hutaki yaani acha tu” alisema


“Haya bana, ushafika nyumbani?”


“Yes nimelala hapa kwa raha zangu huku nikiongea na mtoto mzuri”


“Hahaha….sawa, kesho mimi niko free si tutaonana au?” niliuliza


“Yes, ninalikumbuka hilo, and, muda wote mimi nikogo free, ningetamani pia wewe uache kazi yako tuishi kwa amani muda wote”


“Unachekesha kweli” nilisema


“Nachekesha nini?”


“Niache kazi ili tuwe na muda wa kuwasiliana? Halafu nile nini?”


“Hahaha….unaonekana unakuwa na hasira za haraka, anyway kesho tutaonana asubuhi saa tatu, ndio nataka tukazurure kidogo”


“Wapi?”


“Sehemu nyingi hata Aya Sophia sio mbaya” alisema


“Mh Aya Sophia??” nilimuuliza kwa sababu najua Aya Sophia ni hoteli ya gharama sana”


“Hahaha…kwani vipi?”


“Hoteli ya gharama sana” nilisema


“Hela ya starehe ipo wala usijali” aliniambia


Sikutaka kumuuliza maswali mengi sana kwa sababu nilikuwa ninajua hana maisha, lakini sikujmjadili sana kwani nilihisi ndio maisha anayoyapenda yale ya kula bata


Tuliongea muda mrefu sana, alijua kunibembeleza sana, mpaka nikahisi ni kwa sababu ndio kwanza wageni mapenzi ya kwanza huwa yanakuwa matamu maana kuna kitu kinatafutwa sana, nilisikia burudani kuongea naye lakini bado sikumpa jibu kwamba nimempenda licha ya kwamba yeye alionekana kutamani mimi na yeye tuingie kwenye mahusiano.


Nilikuwa na msimamo mmoja kwamba mimi siwezi nikaachana na Meshack kwa sababu tumetoka mbali, hata hivyo moyo wangu ulikuwa umesharidhika kumpa penzi Rayan lakini nilikuwa namkazia kwa sababu nilikuwa sitaki anione mrahisi


Hata hivyo nilikuwa najua kabisa, akiniomba vizuri ninampa yote maana alikuwa ameshazitengeneza hisia zangu zikawa zinamtaka yeye muda wote kuliko hata Meshack


Saa nyingine nilikuwa najisemea liwalo na liwe mi ninampa tupate raha kwani Meshack atajua? Nikajua ngoja kwanza mambo yetu yakae yanavyotakiwa


Sio siri nilikuwa nimeshamtamani Rayan, nilikuwa tayari kuwa naye lakini sio forever ni kwa ajili ya kujirusha tu na kuinjoy.


*

Kesho yake asubuhi na mapema nilijiandaa, nikaingia bafuni, nikaoga, nikanyoa vizuri ili lolote likienda kunikuta huko nisije nikadhalilika mimi ni mrembo bhana.


Nikampigia simu ili aje anichukue nyumbani maana sikutaka kutembea na gari yangu siku hiyo………ITAENDELEAAA 


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group