MUNIRA AFISA MIKOPO SEHEMU YA 1


 SEHEMU YA 01

Ni miezi miwili ilikuwa imepita tangu Rayan alipokuja ofisini kwetu na kuchukua mkopo wa Tsh laki tano, ambazo alitakiwa kuzirejesha kila mwezi shilingi laki na ishirini kwa miezi mitano ili iweze kufika laki saba.


Hata hivyo Rayan hakuwahi kurudi kabisa baada ya kupokea ule mkopo, na hakuwahi kurejesha hata shilingi mia moja, bossi wangu aitwaye Meshack Mushi akaniuliza “Hivi Munira….huyu Rayan Kazimoto mbona sielewi elewi”


Mimi nilishangaa maana nilikuwa silijui hilo jina katika kukagua sikuwahi kukutana nalo kabisa, nikamuuliza “Rayan Kazimoto ni yupi tena?” 


Meshack akaniambia “Ina maana wewe huelewi kinachoendelea? Ina maana hauko makini na kazi yako?” alisema kwa hasira


“Mh Meshack” nilimtaja jina kwa sababu vile vile Meshack alikuwa ni mpenzi wangu wa kipindi cha miezi sita iliyopita tayari.


“Ah, hizo dharau sasa” alisema “Njoo huku uangalie wadeni wako mnataka kuniharibia ofisi?” aliniuliza


“Hapana boss sifahamu” nilisema huku nikiinuka na kumfuata hadi ofisini kwake, aliketi na kuanza kuchezea mouse ya kompyuta yake ya mezani kisha akaniambia


“Njoo angalia wadeni wako huku na hamfuatilii”


Nilienda mpaka mbele ya kioo cha kompyuta nikatazama, nilipotazama niligundua kweli kulikuwa na kijana ambaye alikuwa amekopeshwa pesa laki tano kipindi cha miezi miwili iliyopita lakini hakuwahi kurejesha na anadaiwa laki saba ya jumla bila kuzingatia faini za kuchelewa kulipa


“Miezi miwili na hatujamfuatilia?” niliuliza


“Ina maana unaniuliza mimi? Hili si ni jukumu lako wewe kaka afisa mikopo au vipi?” aliniuliza


“Samahani boss, ngoja nikatafute faili lake kwenye kabati, ili nipate taarifa zake tuweze kufuatilia kesho”


“Fanya haraka, ikiwezekana, le oleo mjue yuko wapi”


“Sawa”

Niliondoka pale nikaenda hadi kwenye kabati lenye mafaili ya watu wenye mikopo, nikaanza kutafuta kwa namba ambazo kila mdeni alikuwa amepewa.


Nilipokuta lile faili nilishangaa kwani sikuwahi hata kufikiria na mimi kwenye kazi nilikuwa makini sana, nikajiuliza “Sio bure huyu kaniroga” nilisema na kuketi kwenye kiti changu nikaanza kukagua taarifa za yule kijana.


Nilikutana na namba yake ya simu, nikaamua kumpigia moja kwa moja kupitia simu ya ofisini ambayo ilikuwa ni simu janja na sio simu ya mezani kama zilivyo ofisi nyingi.


“Hallo” nilisema


“Hallo mambo vipi?” ilitoka sauti nzito kutoka upande wa pili


“Salama ndugu samahani ninaongea na Rayan Aboubakar Kazimoto?” niliuliza


“Ndio, nani mwenzangu?” aliniuliza


“Mimi ninaitwa Munira, ni afisa mikopo katika kampuni ya LPF”


“Ndio”


“Ni miezi miwili imeshapita tangu ulipochukua mkopo, mbona hujarejesha hata asilimi kumi?” niliuliza


“Mh samahani nitakupigia” alisema na kukata simu yangu


Hasira zilinipanda kwa sababu yeye hakujua kwamba mimi ananiharibia kazi, nilijaribu tena kumpigia lakini hakupokea na hata mwisho akaniweka kwenye orodha nyeusi kabisa ili nikimpigia simu yake iwe kama inatumika muda wote


Nilichukua simu yangu mwenyewe, nikamtumia SMS ya gadhabu nikamuambia “Tafadhali usicheze na kazi yangu, mimi hapa boss ndiye ananisumbua, naomba ufike ofisini leo la sivyo tutakuchukulia hatua” nilisema lakini hakujibu kabisa………….


Basi siku ilipita hakufika ofisini, kesho yake vile vile hakufika nab ado kila nilipokuwa ninampigia alikuwa anatumika.


Nikaanza kuwatafuta wadhamini wake, lakini bado hawakuweza kusaidia kitu chochote.


Ikiwa ni siku mbili baadaye, nilichukua pikipiki ya ofisini ambayo alikuwa akiniendesha kijana aitwaye Kevin nikamuambia anipeleke nyumbani kwa Rayan maana kwenye faili kulionyesha taarifa za alipokuwa akiishi kipindi chote kile.


Tulielekea Kigamboni, halafu tukachukua askari mmoja ili tuende naye kutoka kituo cha pale pale Kigamboni, tukaenda mpaka katika duka lake ambalo lilikuwa lipo Kigamboni, tulipofika dukani pale, tulikuta duka yupo muuzaji na lilikuwa limebaki vitu vichache sana maana yake lilikuwa linaelekea kufa.


Tukamuuliza yule binti “Boss wako yuko wapi?”


Akatujibu “Yuko nyumbani”


“Nyumbani ni wapi?” niliuliza


“Nyumbani sio mbali, ni mbele tu hapo”


“tunaomba utupeleke haraka iwezekanavyo”


Yule msichana alikuwa mtiifu alifunga duka akatupeleka mpaka katika nyumba ambayo alikuwa akiishi Rayan. Ilikuwa ni nyumba ya kupanga, tena zile nyumba za zamani sana.,…………ITAENDELEA



GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA PILI (2)





Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group