MAAJABUA YA MGENI SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI (22)


 Sehemu 22 🔞


Baada ya Mama Zena kufanikiwa kumtoa Henry mpaka nje alifunga geti na dakika hiyo hiyo alimpigia mwenye nyumba kwamba aje amkabidhi nyumba yake, maana alikuwa hayupo tayari kuendelea kukaa tena pale.


Henry akiwa kachanganyikiwa huku anagonga mlango kumuita Mama Zena, mara Isabella alifika dakika ile ile.


"Henry usijali Mimi nipo, ntakusaidia!" Isabella alifika na kumshika Henry.


"Isabella niache bwana utanisaidia nini Sasa!?" Henry aliongea kwa hasira, basi Isabella alitoa kibunda Cha pesa na kumuonesha Henry, yaani binti Isabella kumbe alikuwa kachukua akiba yake yote ya mshahara anao lipwaga na kumletea Henry.

Henry baada ya kuona zile pesa alimwangalia Isabella na kutabasamu, na Henry alikuwa hampendi Isabella hata kidogo sema zile pesa tu ndo zilimtamanisha.


Basi wawili wale walipanda bajaji pale na kuelekea mpaka kwenye guest moja hivi ambayo ilikuwa imejificha kidogo, basi Isabella alilipia chumba Wiki nzima kwamba Henry ndo atakaa pale kwa Muda wakati wanafanya utaratibu.


Huku nyumbani kwa Mr madini kilikuwa kimeumana haswa kati ya Fatuma na Filomena, yaani ulikuwa ni ubishani mwanzo mwisho.


"Filomena unataka uniambie wewe hukujua kama Henry ni shemeji yako, tamaa gani za kijinga hivyo mpaka tunaanza kuonekana Sisi ni wajinga!?"


"Aaaaaa!! Fatuma si yaishe kwani mpaka Baba akute tunabishana hiyo hiyo mada!!?" 


"Haaaaaa!! Filomena ni Bora Baba ajue, maana umezidi na huo ni ukorofi tena ulio pitiliza Wewe unalalaje na bwana Yangu!!?"


"Fatuma kwani Henry ni bwana yako kakuoa!?"


"Eeeeee!! Umeona usivyo kuwa na akili kwa hiyo kama hajanioa wewe unaona ni sawa Mtu na ndugu yake kushare mwanaume!?"


"Eheeee kulikoni hapa tokea nipo nje nasikia makelele, kuna nini!?" Fatuma na Filomena wakiwa wanaendelea kubishana pale Mara Mama Filomena alifika.


"Mama ni Bora umekuja, si huyu mwanao kaenda kunichukulia Henry Wangu, namwambia hapa kwamba alicho fanya sicho naye ananipandishia sauti" Fatuma alianza kutoa maelezo.


"Sasa nyie nisikilizeni nyie ni wasomi na naomba kuanzia dakika hii naongea hiyo mada ikome na Baba yenu asije akajua huo ujinga, na pia kuanzia leo sitaki kusikia kuhusu Henry wapumbavu nyie yaani mnagombana kisa mwanaume!??" Mama Filomena aliongea kwa ukali usio wa Kawaida.


"Aaaaaa!! Mama Mimi Henry siachani naye Labda Fatuma!!?" Filomena aliongea kwa sauti ya Chini chini tena ya manung'uniko.


"Unasemaje Filomena!? Hivi hili litoto lipumbavu eee!! Ndo maana Mimi sipendagi kuitwa Mama Filomena kwa ajili ya upumbavu wako, Sasa wewe neng' eneka nije nisikie upo na Henry tena, haya Huyo Isabella yuko wapi nampigia Simu hapokei!??"


"Mama huwezi Amini Isabella yupo huko anamfuatilia Henry!"


"Heeeee!! Jamani huyo Henry ana nini lakini mbona hivyo, Sasa nasemaje awamu hii Isabella Kazi hana si Baba yenu huwaga anamtetea raundi hii tutaona" mama Filomena aliongea kwa hasira na kuingia ndani.


Basi siku Hiyo ilipita Isabella hakurudi nyumbani, maana alikuwa kanogewa na penzi la Henry mpaka Siyo vizuri.


Siku zote ninge ninge na majuto huwaga vinaanza kuja baada ya hasira kuisha, Mama Zena baada ya hasira kuisha na kulala usiku huo bila Henry alijikuta kama hayupo Sawa hivi, yaani Yeye mwenyewe bila kulazimishwa alianza kumtafuta Henry tena kila kona ya mtaa.


Basi siku mbili zilipita huku Isabella akiwa anakula bata na Henry tu, na kijana Henry alikuwa hana Raha kabisa kuwa na Isabella Sema ni kwa vile tu alikuwa hana Namna, Henry Siku hiyo baada ya kuwaza na kuwazua aliamua kurudi pale alipo kuwa anakaa na Mama Zena, Henry alipiga hodi lakini Cha ajabu ule mjengo Mtu mwingine alikuwa kaingia tayari.

Basi Henry kitu alicho kifanya aliamua kumfanyia Isabella kitu mbaya, Siku hiyo ilikuwa ni Jioni Henry aliingia chumbani wanako kaa na Isabella kwa muda huo, kwakuwa alikuwa kaziona pesa zote za Isabella zilipo Henry alibeba zote na kutokomea.


Isabella alikuwa katoka Kidogo kwenda kununua chipsi na mishikaki na baadhi ya vinywaji wakati anarudi alikuta Henry hayupo, mwanzo Isabella hakushituka kama ndo ashapigwa changa hivi, yeye alihisi Henry kaondoka Mara Moja anarudi ila kadri alivyo zidi kukaa pale ndipo alipo anza kuhisi tofauti.

Isabella alipo kakagua pale alipo kuwa kaweka pesa zote, hakuona hata shilingi kumi, kiukweli Isabella alichanganyikiwa nusura ya kuvua nguo, yaani alilia kilio Cha bila kujua wa kuja kumnyamazisha.


Basi Siku hiyo ilipita huku Isabella akiwa analia usiku kucha, ilipo fika asubuhi tu ilibidi Sasa Isabella ndo arudi nyumbani.

Isabella alifika alikuta familia yote imeketi kwenye meza wakipiga kifungua kinywa huku Mr madini naye akiwepo.


"Isabella ndo unarudi!? Yaani unajiamulia tu kwamba nirudi nisirudi, Sasa sitaki maelezo mengi kabebe mabegi yako chumbani uondoke na kama unanidai nambie nikupe pesa zako uondoke, mabinti wanao hitaji Kazi ni wengi muno" Mama Filomena baada ya Isabella kufika tu alimpa maneno yake.


"Uuuuuuu!!!mama Filomena hiyo siyo haki, yaani hujui Mtu katoka wapi na alipatwa na matatizo gani unafanya maamuzi ya hivyo kwa nini lakini!??"


"Baba Filomena nilijua tu utamtetea, ila nasemaje raundi hii nimeamua Isabella anaondoka utake usitake, wewe unafikri ana Sababu ya msingi Zaidi ya kusema alikuwa kwa mwanaume!" Mama Filomena aliongea kwa ukali.


"Mama Filomena naona Sasa umeanza kuvuka mipaka, unanipandishia sauti Mimi ili iweje!? Haya Isabella haondoki Mimi ndo nimeamua" Mr madini aliongea kibabe kama kichwa Cha familia kweli kweli.


"Baba Filo nimeanza kuwa na shaka kuhusu wewe na Filomena, kwa nini kila Muda unamtetea!?? Yaani Siku nne hajalala nyumbani we unaona sawa tu"


"Mama Filomena wewe fikiria unavyo fikiria ila nimesema Filomena haondoki, yaani binti tumekaa naye Zaidi ya Miaka minne, leo hii kwa Sababu za kijinga tu unataka umfukuze nasema haiwezekani!" Mr madini aliongea kwa msisitizo na ukali baada ya hapo aliondoka.


"Isabella au wewe unatembea na Mume Wangu, maana haiwezekani akutetee kiasi hicho!?" Mama Filomena baada ya mumewe kuondoka alimgeukia Isabella, ila binti huyo hakujibu kitu aliingia chumbani kwake.


Henry naye baada ya kutoroka na pesa za Isabella aliamua kwenda mtaa mwingine wa mbaali kabisa, na alikuwa anataka kutafuta chumba huko ili aanze maisha ya kujitegemea huku akiwa anafanya vibiashara vidogo vidogo, ila bahati mbaya bila kujua mtaa alio hamia ndo kulikuwa nyumbani kwa kina Zena yaani nyumbani kwa Mama Zena.


Basi Siku hiyo ilikuwa Jioni Henry akiwa anazunguka zunguka kutafuta chumba mitaa hiyo, Siku hiyo ilikuwa ni Wikendi Mama Zena na watoto wake naye alikuwa katoka bichi kula upepo ndo walikuwa wanarudi.

Ila wakiwa wanakatiza njia ya kuelekea nyumbani kwao Mara walimuona Henry kwa mbaali akiwa anatembea kuja uelekeo waliko.


"Heeeee!!! Mama si Henry yule Bwana ako au!??"Zena aliongea huku akiwa anamtania Mama yake.


"We Mtoto koma eeee!!! Bwana yangu kutoka lini!? Au unafikri sijui kama ulikuwa na mahusiano naye!?" Mama Zena alimchana ukweli binti yake yaani Zena alibaki kaacha mdomo Wazi tu, maana yeye alijua Mama yake hajui kuhusu yeye na Henry.


"Mama ebu simamisha Gari nikampe hai basi" Zena akiwa anacheka alimwambia Mama yake.


"We mpuuzi nini!!? Alafu Zena naona Siku hizi umeanza kunizoea vibaya eee!? Kwani we wanaume wameisha mpaka Henry pumbavu zako yule naye mwanaume!?? " Mama Zena alimpondea Henry baada ya hapo aliendelea kuendesha Gari, ila Mama Zena naye kiroho kilikuwa kinamuenda sipidi kweli kweli, yaani alikuwa anamtaka Henry isivyo kawaida.


Basi Mama Zena na watoto wake walifika mpaka nyumbani, waliingiza gari kwenye geti na kulipaki, lakini baada ya Zena kushuka tu alichomoka haraka kuelekea barabarani ili kumuwahi Henry, kitendo hicho kilimuuma mama Zena kweli kwa Sababu yeye ndo alikuwa anataka amuwahi.


Henry akiwa hana hili Wala lile huku akiendelea kutembea mara alisikia anaitwa nyuma alipo geuka alimuona Zena.


Zena ilibidi amkaribishe Henry mpaka nyumbani kwao na kweli Henry aliingia mpaka ndani, Henry alibaki katumbua macho baada ya kumkuta Mama Zena mule ndani.


"Henry usivyo kuwa na aibu umeamua Sasa kuja mpaka Kwangu!??" Mama Zena kiroho kikiwa kinamuuma alimuuliza Henry.


"Aaaaaa!! Samahani sikujua kama kwako maana Zena kanileta hajanambia kama ndo nyumbani,basi Mimi acha niondolee" Henry aliongea na kunyanyuka kwenye kiti.


"Henry kaaa basi kwani kakuleta Mama au nimekuleta Mimi!??" Zena ilibidi aingilie kati na kweli Henry alikaa.


"Mama Mimi nimekuja kumtambulisha mchumba Wangu rasmi kwako kama mzazi Wangu, Henry ndo mchumba Wangu atakaye nioa" Zena bila kupepesa macho tena akiwa anajiamini aliongea maneno ambayo Henry mwenyewe alibaki anashangaa, hata Mama Zena naye alibaki anashangaa.


"Zena acha ukichaa! Henry hawezi kuwa mumeo narudia tena Mimi kama Mama yako Henry hawezi kuwa mumeo!?" Mama Zena aliongea kwa msisitizo tena kwa ukali.


"Mama kwa nini!?? Nipe Sababu!?" 


"Nikupe Sababu kwani we hujui nakuuliza we hujui!"


"Ndiyo Mama sijui ndo nataka nijue kwa nini hawezi kuwa mume Wangu!?"


"Zena hivi Siku hizi unakunywa pombe eee!? Henry we hujui kama ni mwanaume Wangu, yaani ulivyo laanika Sasa umeanza kutamani hadi mwanaume wa Mama yako Siyo!??" Mama Zena aliamua kufunguka.


"Mama nawe uwage na aibu basi, mbele ya wanao kweli ni maneno ya kuzungumza hayo, hivi kweli Henry wewe unaona ni umri wako wa kutaka awe mumeo!? Mama unacho fanya sicho tena siyo halali kabisa!" Zena aliongea huku machozi Sasa yakiwa yameanza kumlenga lenga.


Mama Zena alijikuta aibu tu anaona mbele za watoto wake maana naye alijishitukia aliona kaongea upumbavu.


"Zena mwanangu Mimi simanisha kwamba natembea na Henry, ninacho Manisha kwamba unawezaje kuwa na mwanume ambaye nimewahi kuwa naye kwenye mahusiano kipindi Cha nyuma!?" Mama Zena alibadili kauli baada ya kuona amekosea.


"Mama hiyo ishapita! Mimi naangalia tu ya mbele, kikubwa ni heshima tu kwa Saiz Mimi nampenda Henry" Zena aliongea na Mama Zena alitikisa kichwa kuonesha kwamba ni sawa ila ndo roho ilikuwa inamuuma nusura ya kupasuka, yaani alikuwa anamkosa Henry huku anajiona.


Basi  Siku zilizidi kusogea zilipita kama Wiki mbili hivi huku Henry na Zena likiwa penzi Moto Moto, na kipindi hicho Henry alikuwa anakaa nyumbani kwa kina Zena.


Huku nyumbani kwa kina Fatuma mambo yalikuwa yamejibu, Fatuma alikuwa tayari kajulikana kwamba ana ujauzito na baada ya kubanwa na wazazi wake Fatuma hakutaka kuficha alimtaja Henry kama ndo mhusika wa ule ujauzito.


Mambo yanazidi kuwa pambe! Je ipi Hatima ya kijana Henry!??


Itaendelea........


Usikose sehemu ya 23

GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU (23)



Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group