Sehemu 18 🔞
Kwanza Mr madini baada ya kuingia alibaki katumbua macho baada ya kuona sura ya Mama Zena pale kwenye sofa, pia Henry naye alikuwa anawashangaa kina Filomena na kujiuliza kwamba wamefuata nini!!
"Fatuma ndo huyu Mama aliye kuitia askari!??" Mama Filomena aliuliza kwa ukali ila jicho lote lilikuwa kwa Henry.
"Henry kwani vipi hawa ni kina nani mbona sielewi, alafu we Mzee umefuata nini hapa!?" Mama Zena naye aliuliza kwa mshangao.
"Unauliza tumefuata nini, nimemfuata Henry Wangu!" Fatuma aliongea kwa kujiamini, ila Mr madini alikuwa kanywea na hakuongea hata neno, maana alikuwa anamkumbuka vizuri Mama yule.
Kwanza ilibidi Mr madini atoke mwenyewe nje kwa aibu, maana aliona Siri ikitoboka vitaumana.
"We mpuuzi wewe naona unanitafuta, Henry yule mpuuzi aliye toka nje unamjua!??" Mama Zena ilibidi aulize kwa ukali na jaziba, maana alimkumbuka vizuri Mr madini, na Siku alipo wafumania na binti yake hawakumalizana vizuri.
"We unasemaje Mama Zena, Baba Yangu usimuite mpuuzi Sawa eee!??" Fatuma ilibidi adakie juu kwa juu!!
"Ahaaa kumbe ndo upuuzi mnao mfundishaga binti Yangu zena siyo!!? Yaani msivyo na aibu mnakuwadia mwanangu Baba yenu, binti Yangu anaacha masomo anaenda kushinda mahotelini na Baba yenu, we binti kumbe shetani hivyo!?" Kesi iligeuka gafla, yaani Mama Zena aliongea point ambayo ilifanya Fatuma abaki kaacha mdomo Wazi huku akiwa anashangaana na Mama yake.
"Fatuma mbona sielewi huyu Mama anamanisha nini kwanza, mjue mnanichanganya!!?" Mama Filomena naye akiwa haelewi aliuliza, yaani maada ilibadilika gafla, haikuwa tena maada ya kuulizana kwamba kwa nini Fatuma alipelekwa kituoni.
"Mama hata Mimi sielewi kitu chochote anacho zungumza Mama Zena!?" Fatuma alijibu.
Muda huo Mama Zena alipo mwangalia vizuri Mama Filomena alimtambua vyema Kabisa, maana kwa Mara ya kwanza anamuona Henry alimuona akiwa na Mama huyo hotelini.
"Ahaaaaaa nilicho gundua familia yenu ni familia ya ufusika na umalaya, yaani Baba kama watoto na watoto kama Mama tu" Mama Zena akiwa anacheka aliongea kauli ambayo ilifanya Mama Filomena aje juu.
"Mama wewe tuliza mdomo unataka nitoboe Siri zako mbele za watoto wako, au unafikri sijui Siri yako yoyote na naweza kukuumbua ukaumbuka mpaka ukakoma." Mama Zena alimtuliza Mama Filomena.
"Siri gani hiyo mpuuzi mmoja wewe unatukana familia Yangu unasema Siri, alafu huyu kijana si kama mwanao kabisa, huna hata aibu!!" Mama Filomena akiwa anajiamini alitema cheche.
Mama Zena hakutaka kujibu aliingia kwenye Simu yake na kuanza kugau picha ambayo alikuwa kapiga Siku ile usiku Henry na Mama Filomena wakiwa wanatoka pale hotelini.
Mama Zena baada ya kuipata alimvutia Mama Filomena pembeni na kumuonesha ile picha, maana Mama Zena alikuwa anajua akitoboa Siri ile mbele ya mabinti zake hatakuwa kamtendea haki mwanamke mwenzie.
Baada ya Mama Filomena kuona ile picha kwanza alibaki katumbua jicho huku sura ikiwa imemushuka vibaya muno, yaani alipoa gafla.
"Mama Kwani kuna nini kinaendelea mbona hatuelewi!?!" Fatuma aliuliza akiwa kamkodolea Macho Mama yake.
"Fatuma ebu tuondokeni tutaongea nyumbani, si mnajua kuleta vurugu kwa watu hairuhusiwi kisheria" Mama Filomena kiukweli alibaki kama Mchungaji mhubiri Amani.
"Mama Mimi sikuelewi kama wewe unaondoka ondoka ila Henry Wangu Mimi simuachi!!" Fatuma aliongea kwa sauti ya juu.
"We binti sitaki unitafute sawa eeee na pia kuanzia leo sitaki muongee na Mwanangu Zena, yaani urafiki wenu ufe mpuuzi mmoja wewe" Mama Zena aliongea kwa ukali, Muda huo Mama Filomena alitoka nje.
"Fatuma tuondoke basi, si utatumia njia nyingine tu kumpata huyo Henry!!" Filomena ilibidi ambembeleze ndugu yake na kweli Fatuma alikubali kutoka japo kishingo upande, ila binti huyo bado alikuwa kabakiwa na utata kichwani mwake kwamba kwa Nini Mama huyo Kasema wanamkuadia Baba yao mtoto wake.
"Filomena hivi wewe umemuelewa Mama Zena point yake!? Na kwa nini aseme tuache kuongea na Zena!??"
"Fatuma kakwambia wewe na hajanambia Mimi maana wewe ndo rafiki yake na Zena, alafu kingine urafiki wa kinafiki acheni!?"
"Filomena maneno ya kipuuzi sipendi, we si unajua Jinsi gani nilivyo vurugwa, urafiki wa kinafiki we unaujua, ebu naomba kaaa kimya!!"
"Fatuma kwa taarifa yako, Baba anatembea na Zena, na kipindi kile Baba anadai kasafiri alikuwa na Zena wanakula zao raha hotelini, we unafikri Mama Zena kayaanza tu Maneno yale kuropoka" Filomena aliamua kutoboa Siri, kwanza Fatuma aliganda kama kapigwa na shoti hivi, yaani alitamani acheke muda huo huo alitamani alie.
"Filomena una uhakika unacho kiongea!??"
"Heeeee Fatuma unafikri nabunia, au unahisi kwa nini Mimi nimepunguza ukaribu na Zena, unakumbuka kipindi kile Zena haonekani chuo, ndo hicho kipindi alikuwa na Baba, na Mama yake Zena anajua kila kitu ndo maana uliona Baba kanywea baada ya kumuona Mama Zena" Filomena alitoboa Siri.
"Duuuu!! Mdomo koma!! Kweli dunia ina mengi" Fatuma maneno yalimuisha ilibidi akae tu kimya.
Basi familia ya Mr Madini walirudi nyumbani kama mabubu hivi, yaani njia nzima hakuna aliye ongea kila Mtu alikuwa kakaa kimya tu huku akiwa na Siri yake moyoni, ila Siri ya Mr Madini watoto wake tayari walikuwa wanaijua isipo kuwa mkewe.
Huku nyuma naye Henry ilibidi Sasa ambane Mama Zena kuhusu Siri anayo Sema anaijua ya Mama Filomena.
"Dear ebu nambie kitu gani umemuonesha mpaka akanwyea vile!??"
"Henry achana nayo yashapita tuendelee na yetu basi!! Au kama vipi tutoke out!?"
"Ebu niambie basi ni Siri Gani hiyo!? Au huniamini kuna vitu unanificha!?? " Henry alikuwa kakomalia kama ndo anadai Malipo hivi.
Basi Mama Zena ilibidi achomoe Simu na kumuonesha ile picha, yaani Henry alibaki kaacha mdomo Wazi kama kabanwa pumbu na mkasi.
"Heeeee!! Ulipiga lini hii picha!??"
"Henry kama ushajua ni Siri gani basi tuendelee na mengine, au unataka hii picha nikamuoneshe Fatuma na Mr madini!??" Mama Zena Sasa ni kama naye alipata sehemu ya kumkamatia Henry.
Basi kijana Henry baada ya kuambiwa vile alibaki mdogo kama pilitoni vile, yaani alikuwa hapati picha Siku ile picha ikimfukia mwenye Mke wake itakuwaje.
Je ipi Hatima ya yote!??
Itaendelea..............
Usikose sehemu ya 19
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA TISA (19)
