Sehemu 19 🔞
Basi kijana Henry baada ya kuambiwa vile alibaki mdogo kama pilitoni vile, yaani alikuwa hapati picha Siku ile picha ikimfukia mwenye Mke wake itakuwaje.
Basi siku Hiyo ilipita huku nyumbani kwa Mr madini kuanzia Mama mpaka watoto kila Mtu alikuwa anafikiria Namna ya kwenda kumfuata Henry maana kila Mtu alikuwa na shida naye.
"Mama Jana hata sikupenda pamoja na yote, Mimi nilijua tumeenda pale Labda ntaondoka na Henry Wangu, ila sikuelewa hata kilicho endelea maana niliona kila Mtu anatoka tu" basi Siku hiyo ikiwa ni jumapili wakiwa kwenye meza ya chakula Fatuma alianzisha maada huku akiwa analalamika.
"Heeeee!! Fatuma ulimuona Henry!!?' Isabella baada ya kusikia Fatuma kaongea alidakia juu kwa juu, maana naye alikuwa anamsaka Henry kama dhahabu hivi.
"We mpuuzi si endelea kula Henry anakuhusu nini Sasa!! Muone bichwa kubwa kama tikiti we si ndo ulifanya mpaka akakimbia hapa " Fatuma aliamua kumtolea uvivu Isabella, na bahati nzuri Muda huo Mr madini alikuwa hayupo.
"Fatuma mwanangu sikiliza, achana na Henry tafuta mwanaume mwingine mbona wanaume wapo wengi!" Mama Filomena aliongea.
"Mama Mimi mwenyewe namshauri hivyo anakuwa mkali, alafu Fatuma Nicki mbona kijana mzuri tu na bado anakupenda kwa nini usitulie naye!??" Filomena naye alikazia na kila Mtu alikuwa anatetea masirahi yake binafsi.
"Heeeee!! We Filomena ndo ukae kimya kabisa, yaani unataka nimuache Henry ili umchukue wewe, au unafikri sijajua kama na wewe unampenda, kwa taarifa yako kuna Siku nimewahi kuona chati zako wewe na Henry kwenye Simu yako, yaani toka siku ile nina wasiwasi na wewe Filomena!!" Fatuma alifunguka.
"Heeeee!! Filomena ya Kweli hayo!!? Hata wewe unamtaka Henry!??" Mama Filomena aliuliza kwa mshangao maana alianza Sasa kuona kama ule ni ujinga.
"Aaaaa!! Mama siyo kweli, Fatuma anaongea tu uongo " Filomena alikanusha japo ilikuwa kwa mashaka mashaka.
Basi Siku hiyo ilipita ilifika Siku nyingine ambayo ilikuwa ni jumatatu, kama kawaida Fatuma na Filomena walikuwa wanatumia Gari yao Moja kwenda chuo, wawili hao kama kawaida walitoka kuelekea chuo, ila wakati wanatoka tu, Isabella naye alikodi taxi kwa ajili ya kuwafuatilia nyuma, maana alijua tu lazima Fatuma ataelekea huko aliko Henry.
Na kweli kuna Sehemu walifika Fatuma alishuka na kupanda Bajaji huku Filomena akielekea chuoni pekee yake.
Fatuma safari yake ilienda kuishia mpaka pale anapo kaa Henry na aligonga mlango Zaidi ya kugonga ila kwa dalili za pale nyumbani hakuonekana kuwepo Mtu yeyote, ila Isabella baada ya kugundua sehemu Ambayo Henry anakaa aliamua kurudi.
"Akibaki Yangu yote lazima niitumie kulipata penzi la Henry tena na awamu hii hachomoki, lazima nimbebee ujauzito iwe isiwe" hayo yalikuwa ni mawazo ya Isabella akiwa anarudi nyumbani.
Upande wa Filomena naye akiwa anaelekea chuoni Mara alipita sehemu aliona watu wawili wanaingia kwenye Duka Moja kubwa la spea za magari na vyombo vingine vya Moto, Filomena alipo piga macho vizuri alimuona Henry na Mama Zena wakiwa wanazama pale ndani, kwanza ilibidi Filomena apaki Gari pembeni na kutulia ndani ya Gari.
Filomena alikaa kama Nusu saa ndani ya gari, baada ya hapo alimuona Mama Zena anatoka pekee yake na aliwasha Gari na kuondoka.
Filomena aliona ile ni kama ndo fursa yake ya kuongea na Henry, haraka haraka alishuka kwenye Gari na kuelekea pale dukani, alizama mpaka ndani na duka hilo lilikuwa ni kubwa muno.
Filomena alipo piga macho kwa mbele alimuona Henry akiwa anelekezwa mambo na Jamaa mmoja hivi.
"Henry!!!??" Filomena ilibidi aite Kwa sauti!
Henry naye baada ya kugeuka alimuona Filomena, kwanza Henry alichanganyikiwa kumuona Filomena maana aliona binti huyo ni kama anaenda kumharibia.
Haraka haraka alimkimbilia Filomena na kumtoa nje.
"Filomena utaniharibia jamani umefuata nini, hapa mwenzako kwanza ndo leo tu nimekabidhiwa ofisi tena unataka kuharibu mambo gani hayo!??" Henry baada ya kutoka na Filomena nje alianza kulalamika.
"Henry mwanzako nimemiss penzi lako please!!" Filomena aliongea sauti ya mahaba.
"Filomena asubuhi hii mambo ya mapenzi wapi na wapi jamani, Muda wa Kazi huu , we nenda tutawasiliana!"
"Henry tutawasiliana vipi wakati kukupata kwenyewe kwa manati, basi nipe mawasiliano yako Mimi ntakucheki baadae!" Filomena alikuwa anabembeleza kwa sauti ya upole kweli kweli.
(Siku hiyo ndo Mimi huyo nitongozwe na mtoto mrembo kama Filomena tena akiwa anatoka familia ya kitajiri haki ya nani ntaandika historia kwenye dayari 😃😃) Jokes.
Baada ya Henry kuona Filomena anaweza akaharibu ilibidi ampe tu namba, maana Mama Zena alikuwa katoka Kidogo ila alikuwa anarudi na Siku hiyo ndo Siku Henry alikuwa anakabidhiwa mradi Sasa.
Filomena baada ya kupewa namba na Henry na kujua sehemu ambapo anafanyia Kazi kiukweli alifurahi kupita maelezo, ila Filomena alikuwa na wasiwasi kwamba Fatuma anaweza akajua, maana njia Hiyo lilipo hilo duka ndo ilikuwa njia ya kuelekea chuoni.
Filomena alielekea chuo akiwa na Amani muno maana alikuwa anajiona kama mshindi.
Huku kwa Fatuma baada ya kuona geti halifunguliwi ilibidi atulie pale pale getini kusubiri, ila dakika ishirini nyingi Mara Mama Zena na Gari lake alifika, baada ya kuwa kamuacha Henry huko dukani.
"Heeeee we binti wewe hivi una kichwa Cha funza au nini!?? We si ushaambiwa hutakiwi au!? Kwa taarifa yako kwa mambo ninayo mfanyia Henry sidhani kama atakuja kwako, yaani kiufupi karaga bao!!" Mama Zena baada ya kumkuta Fatuma anazengea zengea pale getini bila mpango alishuka kwenye Gari na kumpa makavu yake.
Kiukweli Fatuma aliugulia maumivu ndani kwa ndani na hakujibu kitu, aliamua kuondoka kwa stress tu Fatuma hakwenda chuoni tena alirudi nyumbani.
Masaa yalizidi kusogea huku chuoni Filomena naye mapindi yalikuwa hayapandi yaani Muda wote alikuwa anamuwaza Henry, na alikuwa kamisi shoo za Henry kuliko kawaida.
Siku hiyo ilipita huku Henry akiwa hapokei Simu za Filomena wala kujibu SMS na alipo gundua ni Filomena aliamua kublock kabisa namba ya Filomena, yaani Henry alikuwa hataki kuchezea bahati, maana alikuwa kaonywa na Mama Zena kwamba akija kukutwa na mwanamke yeyote yule basi kila kitu alicho pewa atatapika na pia ile picha itamfikia mpaka Mr madini.
Ikiwa ni Siku nyingine, kama kawaida Fatuma na Filomena walielekea chuo, ila kimakusudi kabisa Filomena kwakuwa alikuwa hataki Fatuma amuone Henry sehemu anapo fanyia Kazi aliamua kupita njia nyingine kwa Sababu Siku hiyo yeye ndo alikuwa kashika uskani.
Basi wawili hao walifika chuo na kuendelea na Vipindi ila ndo hivyo kila Mtu alikuwa na stress zake.
Siku hiyo binti Zena naye akiwa pale chuoni aliona pesa ya matumizi imemuishia na Mama yake alikuwa hapatikani, basi Zena aliamua kwenda kwenye moja ya Duka lao kwa ajili ya kuchua walau pesa, kwa Sababu ilikuwa ni kawaida na miradi yote ni Baba yao alikuwa kaacha.
Kwakuwa Duka la spea za magari ndo lilikuwa karibu na chuo Zaidi, ilibidi Sasa Binti Zena aelekee huko, baada ya kufika tu kwanza alibaki katumbua macho baada ya kumuona Henry yumo mule dukani.
"Heeeee!! Tosi yule pale mshikaji kaanza lini kufanya Kazi hapa dukani!??" Zena baada ya kufika ilibidi aulize.
"Uuuuuuu!! Alianza Jana na yeye ndo Boss Mpya anaye ratibu kila kitu Yaani Mama yako alisema kuanzia Jana kila kitu kinacho husu hili Duka yule jamaa ndo mhusika mkuu" hayo yalikuwa ni maelezo ambayo moja ya mfanyakazi pale dukani alimpatia binti Zena.
"Uuuuuuu!! Huyu mpuuzi atakuwa anajua mambo vilivyo, maana siyo kwa masifa yale aliyo mwagiwa na Fatuma, alafu Mama kabisa ninaye mjua kakamatika hivyo mpaka kaamua kuhonga mradi mkubwa hivi, uuuu siyo bure" binti Zena akiwa anamwangalia Henry alijikuta naye kuna vitamaa vya kijinga vimeanza kumpitia kichwani mwake, yaani alijikuta anatamani kuonja radhaa ambayo Mama yake anaonja.
Kwanza ilibidi Zena amuite kijana Henry na kweli Henry alikuja na walitoka nje kwa ajili ya mazungumzo Zaidi.
Je Henry ndo bahati ya mtende tena au ndo bahati zikizidi mwisho wa Siku inakuwa Sumu!!??
Itaendelea.........
Usikose sehemu ya 20
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA ISHIRINI (20)
