MAAJABU YA MGENI SEHEMU YA KUMI NA TATU (13)


 Sehemu 13 🔞


Muda huo Filomena na Henry nao ndo walikuwa wamepaki Gari yao pale parking na wanashuka kwa ajili ya kwenda kupata chumba kwenye hoteli hiyo, na Siku hiyo Filomena alikuwa kapanga kulala na Henry kabisa bila kujali chochote kitakacho tokea.


Filomena na Henry baada ya kushuka kwenye Gari walibaki wametumbua Macho baada ya kumuona Mr madini akiwa na pisi kali katulia wanacheka huku wanatekenyana!!


"Heeeee!! Jamani naota au!! Yule si Zena yupo na Baba Yangu au!!?" Filomena alijikuta anajiuliza swali ambalo tayari jibu lake analo kichwani.


"Filomena tuondoke haraka tuondoke hapa siyo pa kukaa" Henry aliongea haraka huku akiwa anarudi kwenye Gari, maana Henry aliwaona watu wawili anao wajua, yaani Mr madini na Mama Zena.

Mama Zena naye katika kuangaza angaza baada ya kupiga Macho nyuma kwa macho yake mawili alimuona kipenzi chake Henry akiwa anarudi kwenye Gari haraka haraka.


Mama Zena alibaki njia panda hakuelewa amfuate Binti yake pale alipo kaa au amkimbilie Henry, ila kutokana na nguvu ya mapenzi Mama yule alikimbilia kwenye parking kwa ajili ya kumsimamisha Henry, ila bahati mbaya alikuwa kachelewa maana Filomena aliwasha gari haraka na kuchomoka kwa Kasi pale hotelini, yaani Mr madini na Zena wala hawakuona kwamba kuna watu walikuwa wanamwangalia.


"Jamani Henry why!! Kama nilikukosea si ungesema jamani!? Kipenzi?" Mama Zena alijikuta anabaki analia tu pekee yake pale pale parking, baada ya Mama huyo kufuta Machozi na kukaa sawa Sasa hasira zilianza upya.


"Mpumbavu wewe!! Hasira Zangu zote zinaishia kwako, unamrubuni Binti Yangu anaacha masomo unakuja kumlaza huku" Mama Zena akiwa anaongea pekee yake alianza kutembea kwa Kasi kuelekea pale kwenye gadeni ambapo Mr madini alikuwa kakaa na binti Zena na pia kulikuwapo na watu wengine ambao nao walikuwa wanaendelea na mambo yao.


Watu walishangaa kumuona Mama Zena akiwa anakuja pale huku kakunja sura na anaongea peke yake, yaani Zena na Mr madini walikuja kushituka Mama yule ashafika walipo kaa.


Zena baada ya kumuona Mama yake tu anakuja pale alitoka sipidi za kufa mtu maana alikuwa anamjua Mama yake alivyo kicha, Mr madini yeye alikuwa katulia huku akiwa haelewi mchezo maana hata hivyo alikuwa hamjui Mama mzazi wa Zena.


"Hello!! Zena hei why dear unakimbia!? Zena!?" Mr madini alibaki anaita kwa mshangao pale, ila Kabla hajakaa sawa alirukiwa na Mama Zena Mwilini.


"Pumbavu zako! unasema dear eeee!! Yaani we mpuuzi ndo unamrubuni mwanangu anaacha masomo wewe unakuja kulala naye huku nasema nakuua leo we Mzee wewe" Mama Zena aliongea kwa hasira huku akiwa kamkwida Mr madini kisawasawa.

Yaani Mr madini alikula makofi matatu ya nguvu kutoka kwa Mama Zena, baada ya hapo Mr madini alijitutumua na kumtupa Mama yule Chini,na muda huo tayari watu wa kuachanisha na Walinzi wa pale hotelini walikuwa wamefika.


"Nasema niacheni mpuuzi huyo niache nimunyoshe, haiwezekani nagharamia kumsomesha mwanangu yeye anamrubuni na kuja kulala naye huku hotelini, mjinga nakwambia tutafikishana mbali!!" Mama Zena alikuwa kapatwa na hasira kuu, Siku zote mwizi naye akiibiwa huwaga anaumia kupita kiasi ndo hicho kilikuwa kinatokea kwa Mama Zena, maana Mama huyo alikuwa kazoea kutembea na watoto wa watu, naye awamu hii alikuwa kaminyiwa mtoto wake.


Basi ilibidi watu watulize mambo pale, na kumwambia Mr madini aondoke ili kuepusha ugomvi.

Ni kweli Mr madini aliingia chumbani kwake alikusanya kila kilicho chake na alitoka kurudi nyumbani kwake, maana mambo yalikuwa yameharibika.


Filomena na Henry nao baada ya kutoka pale ilibidi watafute sehemu nyingine ya kulala na walipanga kulala huko huko mpaka asubuhi.


"Filomena kwani yule binti aliye kuwa kakaa na Baba yako pale muda ule unamjua!?"


"Henry ndiyo namjua anaitwa Zena ni rafiki yetu, yaani hata sielewi Baba kakumbwa na nini eti"


"Filomena inabidi tukaushe kama hatujawahi ona kitu, Wala Mama yako usije ukamwambia yaani ibaki Siri yetu sawa eeee!!"


"Henry sawa kwa vile wewe umesema hivyo Mimi nakubali, ila tabia ya Baba kumdanganya Mama Yangu hata sijapenda" Filomena alilalamika kweli Siku hiyo.


Huku nyumbani kwa kina Filomena ikiwa ni Mida ya saa mbili fulani hivi za usiku, Mr madini alifika nyumbani akiwa na hasira hasira tu, maana huko aliko tokea kilikuwa kimeumana.


"Karibu Baba Filomena!! Vipi mbona umekasirika hivyo kwani kuna nini mume Wangu, alafu mbona ulisema unaweza kaaa mwezi na Zaidi mbona mapema hivi umerudi!?" Mama Filomena aliuliza kinafiki, maana Mama Filomena taarifa zote za mumewe kuchepuka alikuwa anazijua japo alikuwa hajagundua kama mumewe katoka kufumaniwa na ndo maana karudi.


"Mama Filomena maswali mengi sipendi, kwanza nimechoka nahitaji kumpumzika" Mr madini alijibu kwa hasira baada ya hapo aliingia chumbani, na Siku hiyo hakuuliza hali za watoto wake kama Siku zingine, kwa hiyo hakujua nani yupo na nani hayupo.


Fatuma naye mapigo ya Moyo yalikuwa yanaenda mbio maana alikuwa anapiga Simu ya Henry pasina kupokelewa, alijaribu kutumia Simu ya Mama yake kwamba huwenda Henry atapokea ila wapi.

Siku hiyo Fatuma aliamua kulala kwenye chumba Henry ili kijana huyo akirudi amkute, kulifika mpaka asubuhi bila Henry na Filomena kuonekana pale nyumbani na wote walikuwa hawapokei Simu, hapo Fatuma alianza kupata mashaka kuhusu Filomena na Henry.


Basi majira ya saa mbili asubuhi Henry ndo alirudi nyumbani, ila Filomena yeye aliamua kupitia chuoni huko huko.


"Henry leo ulikuwa umelala na Filomena siyo!??" Fatuma kwanza ilibidi amvutie Henry chumbani na kuanza kumuuliza maswali huku akiwa kajawa na wivu mkubwa.


"Fatuma acha kuropoka, wewe uliniona wakati nalala naye!?"


"Henry Nahisi hivyo, kwa Sababu wewe hujalala humu ndani pia Filomena naye hajalala Sasa kwa nini nisiwashitukie" 


"Fatuma wasiwasi wako tu Mimi wala sikulala huko unako sema, nililala kwa jamaa Yangu tu baada ya kuona Isabella ananisumbua" Henry aliamua kudanganya na alimchonganisha Isabella.


"Henry!! Henry!! Henry uko wapi!??" Henry akiwa anaendelea kubishana na Fatuma kule chumbani Mara alisikia sauti ya Boss wake Mr madini.


"Heeeee!! Fatuma inamaana Baba yako karudi!?" Henry aliuliza kwa mshangao kweli kweli maana alikuwa hategemei kama Mzee tayari karudi.


"Ndiyo alirudi Jana Usiku" Fatuma alijibu ila ndo hivyo alionekana hana furaha.

Henry ilibidi aitikie wito anako itwa, ila ndo hivyo alikuwa kashajua kwamba huwenda Boss kule aliko kuwa mambo yaliharibika, japo kuwa Henry alikuwa hajui kama Mama Zena yule mchepuko ndo Mama wa Zena yule aliye kuwa kakaa na Boss wake.


"Henry sikiliza Saiz Hamna kutoka toka hapa nyumbani, mafundi wanaanza Kazi leo kwa ajili ya kuzungusha geti hapa nyumbani kwa hiyo stoo ya vifaaa utasimamia wewe, Sasa ole wako mambo yaende tofauti!" Mr madini alitoa Amri na alikuwa anaongea kwa hasira hasira tu.

Basi Henry aliitikia kwa adabu kuu ila moyoni aliona ni upuuzi kuendelea kufanya Kazi pale wakati analiliwa na kila Mtu.


Basi ni kweli mchana mafundi walifika pale nyumbani kwa ajili ya kupima pima, ila Henry yeye alikuwa kaondoka kwenda kudhurura.


Jioni ilifika Filomena alirudi alikuta Fatuma kavimba pale nyumbani kwa hasira mpaka siyo vizuri.


"YuhuFilomena naomba uwe Mkweli leo wewe ulilala na Henry!!??" Yaani Kabla Filomena hajatulia vizuri alidakwa juu kwa juu na Fatuma na kuanza kuulizwa maswali.


"Fatuma mazoea ya kipuuzi sipendi aisee aliye kwambia nililala na Henry nani!??"


"Filomena unajifanya mjanja eee!! Sasa wewe ruka ruka nije nikunase na bwana angu hapo ndo utanijua Mimi kurwa na wewe doto!!" 


"Hahaaaaaaa!! Fatuma acha kunitisha! Eti bwana ako umemuwekea alama, usinitishe mie" Filomena Siku hiyo naye alijikakamua na kumjibu Fatuma kwa nyodo.


"Eheeee makelele ya nini nyie!??" Wakiwa wanabishana pale sebuleni Mara Mr madini aliingia na kuuliza.


"Aaaaa!! hamna Baba hatubishani!" Fatuma akiwa anacheka cheka alijibu.


"Wanamgombania Henry hao hawana lolote" Isabella baada ya kuona Sasa fursa ya kuvuruga imepatikana akiwa jikoni aliropoka.


"Heeeee!! Isabella ebu njoo huku utoe maelezo vizuri, au sijasikia vizuri!?" Mr madini baada ya kusikia kauli ya Isabella kule jikoni aliuliza kwa sauti ya juu, na kweli Isabella alikuja pua ikiwa juu juu, maana alijua wawili wale wakipigwa marufuku kuwa kwenye mahusiano na Henry basi ndo chansi yake, yaani alikuwa hana wazo jingine kwamba Labda Mr madini anaweza kumfanya Henry kitu kibaya.


"Ndo kama nilivyo sema Fatuma ana mahusiano na Henry na ndo maana anamlaumu Filomena, maana naye Filomena anaonekana anampenda Henry" Isabella bila kupepesa macho alitumbua jipu.


Muda huo huo Henry naye ndo alikuwa anaingia mule ndani akiwa anapiga piga vimuruzi huku anachombeza na nyimbo za bongo fleva.


Vipi Henry ndo kakamatika au mbio zake bado hazijaishia ukiongoni!?


Itaendelea..........


Usikose sehemu ya 14


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU SEHEMU KUMI NA NNE (14)


Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group