Sehemu 17 🔞
Muda huo shughuli hiyo inaendelea pale sebuleni na miguno ya mahaba ikiwa imepamba Moto, Fatuma alikuwa anasikia kule chumbani yaani Moyo ulikuwa unamuuma nusura ya kupasuka, alijikuta Sasa kaanza kupata mawazo ya kutoka huku akijisemea kwamba liwalo na liwe.
Shughuli ikiwa imepamba Moto Mara Mama Zena akiwa kaegeshwa kwenye Kochi alishangaa Mtu anajitokeza pale sebuleni.
"Heeeee!! Henry nani Huyo!!!" Mama Zena aliongea kwa mshangao, Henry naye alipo geuka alishangaa kumuona Fatuma.
"Heeee Fatuma ndo nini Sasa!!!??" Henry aliuliza kwa mshangao huku hisia zote zikiwa zimepotea, yaani aliacha hata kile alicho kuwa anakifanya.
"Henry hata kama ungekuwa wewe ungeshindwa kuvumilia, mwenzako uvumilivu umenishinda ! Henry nashindwa kuvumilia mwenzako nakupenda eti!!" Fatuma alianza kuongea huku akiwa anamwaga chozi, muda huo Mama Zena alikuwa anashangaa.
"Henry!! Inamaana huyu binti alilala humu ndani!!?" Mama Zena aliuliza kwa mshangao.
"Aaaaa!! Jana wakati unatoka na Gari bahati mbaya aliingia na alikatalia Humu Humu ndani " Henry Sasa ilibidi amruke Fatuma, maana ukweli ni kwamba kwa Muda huo kilicho kuwa kinatakiwa ni pesa na siyo upendo, kwa hiyo Henry aliona ni bora achague pesa kwanza.
"Henry!! Kwa nini lakini kwa hiyo huyo Mama ndo wa umuhimu kwako, Mama Zena tafadhali naomba niachie mchumba Wangu nipo tayari kufanya lolote " Fatuma akiwa analia alipiga magoti na kuanza kumbembeleza.
"Henry au ulilala naye huyu mpuuzi na ndo maana ulikuwa unanisugua kwa uchovu, mbona sielewi hili picha!??" Mama Zena alianza kushitukia mchezo.
"Aaaaaa!!! Dear Mimi siwezi fanya hivyo, ni kwamba huyu alikatalia humu ndani na nimejaribu kutumia kila njia kumtoa kagoma" Henry alizidi kushikilia msimamo wake.
Mama Zena ilibidi afanye maamuzi magumu, pale pale alitwanga Simu kituoni na kutoa taarifa kwamba nyumbani kwake kuna kibaka analeta vurugu.
"Dear tungemtoa tu kistaarabu!! Fatuma askari wanakuja ondoka basi" Henry alijikuta Sasa anaanza kumuonea huruma Fatuma.
"Henry wewe si umesema hakuna kinacho endelea kati yako na huyu basi subiri askari waje wamzoe akapumzike kituoni kwanza" Mama Zena akiwa siliasi aliongea, na kweli ndani ya dakika ishirini askari watatu walifika pale nyumbani.
Mama Zena alitoa maelezo anayo yajua yeye kumhusu Fatuma, na binti huyo alibebwa juu kwa juu mpaka kituoni, Henry kile kitendo kilimuuma ila ndo hivyo hakuwa na Cha kufanya.
Masaa yalizidi kusogea na Siku hiyo ilikuwa ni jmosi, familia ya Mr Madini ikiwa kwenye meza ya chakula Cha mchana Mara Simu ya Mr Madini iliita.
"Hello mheshimiwa za Siku nyingi bwana!!?" Mr madini alisikia sauti ambayo hakuitambua maana namba ilikuwa mpya, na watu wote pale mezani walikuwa wanasikia mazungumzo hayo.
"Uuuuuuu Salama ndugu Yangu, sijakutambua nani mwenzangu!??"
"Aaaaaa!! Ndugu Yangu ushafuta namba nini, unaongea na afande shayo hapa!!"
"Ohoooo afande vipi bwana za masiku!??"
"Aaaaaa!! Salama, Sasa ndugu Yangu binti yako kaletwa hapa asubuhi afande wenzangu wamemkamata nasikia alienda kwenye mji wa watu kufanya vurugu, kama unaweza njoo hapa kituoni tuyamalize basi" hizo ni taarifa ambazo kila Mtu alisikia, kwanza Mama Filomena aliachia kijiko Cha wali na kurudisha nyama kwenye Sahani.
"Heeeee!! Baba Filo ebu nielezee vizuri, Fatuma kakamatwa, ebu twende haraka!!" Mama Filomena alichachawa baada ya taarifa zile.
"Mama Filomena mbona unapaniki hivyo, Sasa taarifa umepewa wewe au nimepewa Mimi!?? Ebu tulia naenda Mimi" Mr madini alimtuliza mkewe!!
"We mwehu nini, yaani binti Yangu yupo kituoni unaniambia upuuzi, nataka nikajue mjinga gani anadiriki kumuwekea mwanangu nuksi, Filomena ebu kalete funguo kule chumbani juu ya kabati"Mama Filomena alikuwa kapaniki hatari, na Mama huyo ilikuwa Bora uguse watoto wake wengine ila Siyo Fatuma, yaani alikuwa anampenda kupita kiasi.
Basi Mama Filomena na Filomena waliongozana kwenda kituoni huku naye Mr madini akiwa anafuata na Gari yake nyuma.
Basi watatu wale walifika kituoni na kweli walikuta binti Fatuma kawekwa korokoroni huku akiwa kapigwa virungu viwili vitatu kutokana na ubishi ambao alikuwa kauleta wakati anakamatwa.
"Afande ebu naomba nipe maelezo, kwa nini binti Yangu kapigwa hivi, hata kama ni kosa kafanya nyie mna haki gani ya kumpiga mwanangu!?? Nasemaje hii kesi inafika mpaka kwa waziri mkuu, sikubali" Mama Filomena aliwasha moto pale kituoni, yaani Fatuma alikuwa kapigwa kidogo tu, ila Mama huyo alivyo kuwa anakuza mambo kama ndo kupigwa mpaka kang'olewa meno.
Basi Mr madini aliulizia chanzo Cha binti yake kuletwa pale, baada ya kupewa maelezo yote ilibidi Sasa amgeukie binti yake kumuuliza.
"Baba Mimi nilikuwa napambania penzi langu kwa Henry kiukweli Mimi toka Moyoni nampenda, lakini kuna Mama sijui katokea wapi kanichukulia mchumba Wangu alafu ananitishia!!" Fatuma alitoa maelezo ambayo kila Mtu alibaki anashangaa, yaani Mama Filomena ilibidi kwanza atulize mizuka ili kujua kijana huyo yuko wapi, maana naye alikuwa anamsaka bila mafanikio, pia naye Filomena alikuwa anaomba kimoyomoyo ajue ni wapi Henry yupo.
"Heeeee!! Haiwezekani yaani Sababu za kipuuzi hizo ndo zikafanya ukakamatwa, Fatuma ebu twende kwa huyo mpuuzi tukamuulize vizuri" Mama Filomena ilibidi Sasa atumie akili ili ajue ni wapi Henry wake anakaa.
"Okay!! twendeni huko huko, afande shayo nashukuru Ndugu Yangu tutawasiliana basi Kwa Lolote lile" Mr Madini naye aliunga hoja ya Mama Filomena bila kujua Lengo la Mama huyo.
Basi Mtu nne walitoka pale kituoni kuelekea huko inako daiwa kwamba Henry ndo yupo.
"Huku nyumbani kwa Henry baada ya kula chakula Cha mchana na Mama huyo walikuwa wametulia wanacheza karata sebuleni huku wakiwa wameweka mziki kwa mbaali, yaani ilikuwa burudani haswa.
"Hivi Henry nikisema tufunge ndoa uwe mume Wangu rasmi unaweza kubali!??"
"Uuuuuuu!! Kwa nini Sasa jamani nikatae, alafu kwa Nini umewaza hivyo dear!?"
"Aaaa!! Henry naona kama ntakuja kukukosa hivi, maana naona watu wanavyo kunyemelea nyemelea, nilitaka nikumiliki kihalali kabisa, ili Mtu akijichanganya iwe halali Yangu kumfanya ndafu!!"
"Hahaaaa My love hata usijali Mimi ni wako bwana siwezi kwenda popote, hata kama ni ndoa kwangu ni Sawa tu"
"Uuuuuuu!! Sawa wewe unaweza kubali lakini huyo Bibi yako unaye msema anaweza naye kubali!??"
"Heeeee!! Jaman Sasa Bibi akatae kwa ajili ya nini, na kwa mfano ndo ukamwambia unamjengea nyumba! Hahaaa mbona atakupa Baraka zote "
"Duuuu!! Henry yaani mwenzako ningekuwa na uwezo wa kushika ujauzito, haki ya Mungu ningekuzalia, sema ndo hivyo kaumri nako tatizo "
"Usijali dear Mimi......." Mazungumzo matamu yakiwa yanaendelea pale sebuleni Mara honi ilisikika kwa nje tena ilikuwa inapigwa kwa vurugu.
Basi ilibidi Henry atoke mpaka nje kwenda kuona ni mgeni gani kaja kishari vile, Henry alipo fungua mlango tu aliona Sura ya Mr Madini, kwanza Henry ilibidi akimbilie ndani haraka haraka maana alijua Mtu huyo kaja kwa Shari.
"Henry vipi kuna nini mbona unakimbia!??" Mama Zena baada ya kuona Henry anaingia kwa Kasi aliuliza, lakini Kabla Henry hajajibu, Mara kundi la watu kama wanne hivi walingia mule ndani.
Kwanza Mr madini baada ya kuingia alibaki katumbua macho baada ya kuona sura ya Mama Zena pale kwenye sofa, pia Henry naye alikuwa anawashangaa kina Filomena na kujiuliza kwamba wamefuata nini!!
Mambo yanazidi kunoga, upi mwisho wa picha hili!?
Itaendelea...........
Usikose sehemu ya 18
GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA NANE (18)
