MAAJABU YA MGENI SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)


 Sehemu 11 🔞


"Henry!! We Henry wewe!!?" Kijana huyo akiwa anazunguka huku na kule Mara alisikia sauti ya Mtu ikiwa inamuita kwa nyuma, Henry alipo geuka alishangaa kumuona Mama Filomena.


"Henry jamani ni wewe au naota!??" Mama Filomena aliongea kwa Furaha na kumkimbilia Henry pale alipo kuwa kasimama.


"Aaaaaa! ni Mimi mama shikamo!" Henry alisalimia ila Mama yule bila hata kuogopa alimkumbatia Henry kwa Furaha.


"Henry kwa nini uliamua kunikimbia bila kuniaga mwenzako jamani!??" Mama Filomena aliongea mpaka Machozi yalianza kumlenga lenga.


"Aaaaaa!! Isabella ndo alifanya nitoroke, maana kila Siku alikuwa ananitishia kwamba atamwambia Mzee, yaani kila Siku ndo ilikuwa Kazi na Siku ile alinitishia kwamba anamwambia Mzee ndo maana nilikimbia " Henry alitoa maelezo.


"Isabella!!! Isabella!! Sasa wewe subiri alicho kuwa anakitafuta atakipata, haiwezekani Mimi nikonde kwa mawazo Kumbe chanzo ni yule mpuuzi, Henry nakuomba rudi nyumbani basi kama ni mshahara Mimi ntakuongezea!!" 


"Aaaaaa!! Mama Filomena Mimi siwezi kurudi tena kwako, Labda nitafutie Kazi nyingine tu " Henry aliweka msimamo wake, maana maswala ya kutishwa hakuyataka tena.


"Okay basi ntakupa Kazi kwenye maduka Yangu ya vitenge utakuwa unauza pale na wenzako waliopo, ila Kabla ya kukupeleka huko naomba twende nyumbani ilimladi isije ikajengeka picha mbaya!"


"Aaaaaa!! Sasa Mimi ntamjibu Mzee kwamba nilikuwa wapi!??" 


"Henry usijali Mimi ntajuwa Namna ya kukutea " Mama Filomena alizidi kumushawishi kijana.

Wakiwa wapo pale mida ile bahati mbaya Fatuma na Filomena nao ndo walikuwa wanarudi toka chuo,na walimuona Mama yao akiwa kasimama na Henry.


Fatuma na Filomena walisimamisha Gari haraka, yaani Fatuma bila kujielewa alitoka sipidi ya kufa Mtu kutoka kwenye Gari mpaka pale alipo Mama yake na Henry, Fatuma alimkumbatia Henry kwa hisia kali muno, mpaka Mama Mtu alibaki katumbua macho.


"Henry mzima kweli wewe baba!!?" Fatuma akiwa anatoa Machozi kwa Furaha alimuuliza Henry huku Mama Filomena na Filomena wote walikuwa wanashangaa na kila Mtu Moyo wake ulikuwa unamuenda kwa sipidi.


"We mpumbavu ndo nini hivyo huogopi hata watu unamkumbatia tu, alafu kuna ajenda gani kati yenu wawili!??" Mama Filomena Moyo ukiwa unamuenda Kasi aliuliza kwa ukali.


"Aaaaa!!..aaaa. hapana..aaa!!" Henry alijikuta mdomo unakuwa mzito kujibu.


"Mama Henry ni mchumba Wangu ndiyo na ndo atakaye nioa " Fatuma bila kuhofia lolote alitoboa ile Siri, Mama Fatuma alibaki kaacha mdomo Wazi kwa maneno yale ya binti yake, kwanza ilibidi amuwashe Kofi Fatuma kumuweka Sawa.


"Pumbavu dakika hizi naongea naomba muende nyumbani, mtoto mpumbavu wewe unaacha kuwaza masomo unawaza wanaume " Mama Filomena alipatwa na hasira ya ajabu kweli kweli.


"Mama Mimi Saiz ni Mtu mzima nina haki ya kuwa kwenye mahusiano, na Henry ndo Mtu niliye mchagua hata unifanyaje hapa siondoki bila Henry Wangu, Filomena we tangulia nyumbani "Fatuma akiwa siliasi alimjibu Mama yake.


Yaani Mama Filomena Miguu yote ilikuwa inatetemeka alikuwa anaona Sasa ni kama anaenda kumkosa Kijana huyo, pia naye Filomena mapigo yake ya moyo yalikuwa yanaenda kasi ya ajabu maana naye alikuwa kaanza kumpenda kijana Henry.


"Fatuma sikiliza Baba yako akijua huo ujinga unao usema, basi ujue utamuweka kijana wa watu kwenye matatizo hata we mwenyewe nadhani unamjua Baba yako " Mama Filomena ilibidi Sasa aanze kumtisha binti yake.


"Mama!! Huyo Baba Labda umwambie wewe,ila nina Imani hatajua kitu" Fatuma alijitia Moyo, basi Kwa umoja wao walimshawishi Henry kurudi nyumbani na kweli kijana huyo alikubali japo kwa shingo upande, yaani alikubali ilimladi tu maneno yasiwe mengi ila kichwani mwake alikuwa kapanga kutoroka Muda wowote, maana kama ni mdhamini alikuwa kapata mwingine.


Mama Filomena alivyo fika tu na Henry pale nyumbani alikuta mumewe ndo anajianda kuondoka.


"Baba Filomena kulikoni mbona begi tena!??"


"Mke Wangu huwezi kuamini kuna dharura imetokea, nasafiri kidogo na naweza kaaa mwenzi mzima maana kuna mambo yametokea huko ya kibiashara, na pia....... " hayo yalikuwa maneno Mr madini, ila Kabla hajamaliza kuongea alimuona Henry anaingia mule ndani.


"Heeeee Fatuma mumemtoa wapi huyu kenge!?" Mr madini aliuliza kwa mshangao maana ni Siku tano Henry alikuwa hajaonekana pale nyumbani.


"Aaaaa!! Baba eti alikuwa Kijijini!!" Fatuma alijibu.


"Heeeee Kijijini ndo anaenda bila kuaga!?"


"Aaaaaa!! Baba!!!, Henry kasema alimuaga Mama eti!!" Fatuma alizidi kudanganya na tayari walikuwa wamepanga uongo wa kuja kuongea.


"Mama Filomena inakuwaje haya mambo mbona hukusema kama Henry kaenda Kijijini na Mimi tayari nishaagiza atafutwe Kijana mwingine wa Kazi!??"


"Aaaaaa!! Baba Filomena ni kweli aliniaga, ila sikujua kama ataondoka mapema vile, maana aliniaga kwamba anaondoka Wiki lijalo, kumbe eti alipigiwa Simu ya gafla kuhusu Bibi yake kuumwa ndo maana akaondoka gafla" Mama Filomena aliongea uongo, hapo Mr madini ilibidi akubali tu ila yote ilikuwa ni kutokana na haraka ambayo alikuwa nayo.


Mama Filomena alifurahi kweli mumewe kuondoka maana aliona ndo fursa ya kumfaidi kijana Henry, ila alipo kumbuka maneno ya binti yake Fatuma basi alibaki anachoka haswa.


Isabella naye alipo fika nyumbani alishangaa kumkuta Henry asharudi, yaani Isabella moyoni alifurahi alibaki anacheka tu pekee yake.


"Isabella kesho fungasha virago vyako urudi Kijijini kwenu sawa eeee na kama huna pakwenda nenda hata kwenye vituo vya kulea watu wasio na makazi ila siyo hapa Kwangu " bila kupepesa macho baada ya Isabella tu kuingia, Mama Filomena alimchana makavu Isabella.


"Mama Sasa Mimi kosa langu lipi jamani!!" Isabella alijikuta anaanza kumwaga chozi, kwanza Mama Filomena ilibidi amvutie nje.


"Pumbavu zako wewe ndo wakusababisha Henry akimbie hapa nyumbani kwa vitisho vyako!??" Baada ya kufika nje Mama Filomena alianza kumufokea Isabella.

Basi binti Isabella aliomba msamaha na kukiri kwamba hatorudia tena huo ujinga, na kweli Mama Filomena alimsamehe na kumpa onyo.


Basi zilipita Siku karibia kama tatu huku Henry akiwa Sasa analala na Mama Filomena kwa Siri katika ile ile hoteli, na pia alikuwa anakutana na Fatuma kwenye logde yao ile ile, pia naye Filomena alikuwa anakutana na Henry kwa njia anazo jua yeye.

Yaani Henry alikaa wiki moja pale nyumbani kwa kina Fatuma huku akiwa anahudumia Mama na watoto kwa nyakati tofauti tofauti.


Kutokana na kwamba Fatuma alikuwa kajitambulisha kwa Mama yake na kwa ndugu zake kwamba Henry ni wake, basi yeye alijikuta hata akiwa pale nyumbani anajiachia na Henry kama mumewe vile, na kitendo hicho kilikuwa kinamuuma muno Filomena na Mama Filomena.

Binti Isabella yeye ndo alikuwa katengwa na Henry, yaani binti wa watu kila Siku alikuwa haachi kuomba na kumbembeleza kwa kijana Henry lakini kijana huyo ni kama alimfungia vioo kabisa Isabella.


Ila lengo la Isabella lilikuwa ni kunasa ujauzito endapo atapewa chansi na Henry hata Mara Moja.

Basi Siku zilizidi kusogea Hatimaye Wiki mbili zilipita, Siku hiyo ilikuwa Usiku familia ikiwa imekaa kwenye meza ya chakula, Mara Simu ya Mama Filomena iliita na mpigaji alikuwa ni rafiki yake ambaye maduka yao yalikuwa yanakaribiana.


"Hello Mama Filomena mzima weye!??" Baada ya Mama Filomena kupokea Simu alipewa Salam.


"Safi tu shoga Yangu, kwema kweli huko!?? Maana naona Simu usiku usiku Saiz!?" Akiwa hana hata wasiwasi na Simu ile Mama Filomena aliuliza.


"Shoga Yangu, Mumeo kwani vipi yupo nyumbani kweli huko, maana ni Wiki na kitu Sasa namuona kwenye moja ya hoteli mitaa ya huku kwetu" hiyo ilikuwa ni maada Mpya ambayo Mama Filomena aliletewa na shogà yake.


Kwanza ilibidi Mama huyo aingie chumbani kwenda kuongelea mada hiyo, maana aliona kuongea mbele ya watoto hailipi.


"Ebu nielezee vizuri umesema yupo kwenye hoteli ipi na yupo na nani!?"


"Mama Filomena, mumeo yupo hapa hotelini ni Wiki Sasa namuona, na inaonekana analala na kibinti kimoja hivi cheupe chembamba kirefu, kama siyo chanafunzi hiki Kitoto sijui" hayo yalikuwa ni maneno ambayo yalifanya Mama Filomena atoe jasho mule chumbani.


"Sasa shoga Wiki nzima wewe unaenda hotelini kufanya nini mpaka ukamuona mume Wangu!??" Mama Filomena aliuliza kama ndo haamini hivi, maana alikuwa hajawahi fikiria kama mumewe anaweza fanya vitu vya kipuuzi hivyo.


"Eeeeee!! Shoga Yangu kama huamini basi, maana naona Sasa tumeanza kufanyiana upelelezi" basi Mama yule aliongea na kukata Simu, Mama Filomena kwanza alijikuta anacheka pekee yake, maana alijua yeye ndo anachepuka kumbe na mumewe naye alikuwa anachepuka.


"Hiii kweli ngoma droo!! Sasa hapa nimepata Sababu ya kuendelea kula raha na Henry"Mama Filomena alijisemea kimoyomoyo na kutabasamu, baada ya hapo alirudi kwenye meza ya chakula, kufika pale mezani alikuta kuna ubishani wa kufa Mtu.


"Isabella nimekwambia acha kumsumbua mpenzi Wangu sawa eee, lasivyo kazi itakushinda"


"Fatuma kwani wewe ndo ulianza na Henry au ni Mimi!!? Au kisa wewe mtoto wa tajiri!?"


"Hiyo hainihusu ila ninacho taka kukwambia Henry ni Wangu na Mimi ndo mkewe, lasivyo kitu ntakacho kufanya utashangaa " hayo yalikuwa ni mabishano ambayo yalikuwa yanaendelea pale sebuleni kati ya Fatuma na Isabella, Muda huo Filomena na binti Edina walikuwa wamekaa tu kimya.

Basi Mama Filomena ilibidi awe mkali na kuamulia ule ugomvi, Isabella kwa hasira alijikuta anataka kutoboa Siri ya mahusiano yaliyopo kati ya Mama Filomena na Henry, ila kuna kitu kilimwambia vunga kwanza.


Basi kwa Mara ya kwanza Fatuma aliacha chumba wanacho lala na Filomena na mdogo wao Edina, yeye alienda Kulala chumbani kwa Henry na Siku hiyo Mama Filomena alisuburi pale hotelini bila kuona Mtu mpaka aliamua kurudi nyumbani usiku ule mida ya saa sita baada ya kuona Henry haji.


Mama Filomena baada ya kufika nyumbani alipitiliza Moja kwa moja chumbani kwa Henry ili kujua kijana huyo kwa nini hajatokea sehemu wanapo kutanaga.


Je upi mwisho wa yote!??


Itaendelea...........


Usikose sehemu ya 12


GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12)


Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group