MAAJABU YA MGENI SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE (24)


 Sehemu 24 🔞


Ila kwa uoga ambao Filomena alikuwa nao likija swala la kupigwa, Kabla hata hajaanza kupigwa alitaja haraka haraka na alimtaja Henry, kwanza Mr madini alidondosha mkanda kwa mshangao baada ya kusikia Jina la Henry likitajwa kwa Mara nyingine.


"Ebu rudia tena umesema nani!!? Henry au sijasikia vizuri!?" Akiwa anatetemeka kwa hasira aliuliza.


"Aaaaa!! Eeeeee!! ndi! ndi!! ndiyo!! Baba ni Henry!!" Filomena Alijibu huku akiwa anatetemeka.


Kwa hasira Mr madini aliingia chumbani alitoka na bastola na kuichomeka kwenye mkanda.


"Haki ya Mungu Henry nikimpata namshuti risasi ya kichwa tena mchana kweupe" Mr madini kwa hasira akiwa kashika bastola mkononi aliongea, yaani mpaka Mama Filomena aliogopa kumsogelea mumewe kwa hasira ambazo alikuwa nazo, Mr madini alitoka pale nyumbani akiwa anaongea pekee yake.


"Filomena ndo nini Sasa hivyo, nilikwambiaje, unaona Sasa wewe mtoto mbona una kichwa kigumu hivyo, kwa hiyo umeridhika Sasa ulivyo mtaja Henry, nakuuliza umeridhika, au huoni kama Baba yako anaenda kufia Jera kwa maamuzi ya kipuuzi atakayo yafanya!!!?" Mama Filomena alianza kumlaumu Filomena.

Muda huo Isabella naye alikuwa na mawazo kibao na alikuwa anaombea isiwe kama alivyo kuwa anataka mwanzo, yaani Isabella tokea mwanzo alikuwa anaomba apate ujauzito wa Henry, ila baada ya kuona Sasa Fatuma na Filomena wote wana ujauzito wa Henry aliona Sasa malengo yake ya kuishi na Henry hayawezi kuwa kama alivyo kuwa anataka.


Basi siku mbili zilipita huku Mr madini akiwa kaajiri vijana kumsaka Henry kila kona ya mtaa.

Huku upande wa Henry ni kama mambo yalikuwa yanazidi kuharibika, maana Henry ni kama Sasa alianza kisimangwa na Zena kwa ile tabia ya kuwa penda penda hovyo.


"Henry Mimi naona ni Bora tuachane tu, ila kitu ambacho nataka ujue Mimi nina ujauzito wako, ila kwa hizo tabia zako za kuwa na tamaa za kijinga Mimi naona kila Mtu awe kivyake" basi Siku hiyo Zena alikuwa anamchana Henry makavu yake pale nyumbani.


"Zena lakini si tumekubaliana kwamba ntajirekebisha na tutaenda kutafuta sehemu ya kuishi ili Mama yako asiendelee kunisumbua au!!?" Henry naye alikuwa anajitetea.


"Henry tatizo siyo Mama Yangu, tatizo ni wewe, kwani wewe kumkatalia Mama Yangu unashindwa!? Henry nimegundua wewe ni mwanaume mwenye nyege nyingi yaani kila mwanamke akikuvulia chupi tayari unataka kuonja, Sasa Mimi kwa tabia hiyo Sioni kama tutawezana " Zena alikuwa anaongea ukweli Mtupu, maana Henry alikuwa hajui kukataa.


"Kwa hiyo Zena ndo hunitaki tena ama!?" Henry aliuliza kwa kujiamini, na Henry alikuwa anauliza hivyo kwa Sababu alikuwa anajiamini kwamba anapendwa na wanawake kibao.


"Henry ndiyo Mimi naona kila Mtu ale kona yake, Henry siyo kwamba Mimi labda inaniuma wewe kuwa na wanawake wengine, kwa Sababu huwenda hata Mimi nachepukaga ila kinacho niuma kwani lazima awe Mama Yangu!??"


"Zena umesahau kipindi Cha nyuma uliniambia nini?? Nilivyo kwambia Mimi ni mwanaume wa Mama yako!? We si ulisema hujali na kitu unacho angalia ni kama kitu inazama tu, eheee!leo hii imekuwaje!??" 


"Henry hata kama nilisema hivyo nakubali nilikuwa mjinga, ila ujinga haudumu Saiz nishajua nilifanya makosa ila siwezi endelea kushea na Mama Yangu "


"Okay Zena kama umetaka tuachane poa tu " 


"Henry ndo hivyo nyumbani kwetu utoke ndiyo, ukatafute pa kuishi " wawili hao wakiwa wanaendelea na mazungumzo pale nyumbani Mara Mama Zena alifika mule ndani akiwa anahema.


"Duuuu!! Henry ushayakanyaga nakwambia unasakwa huko mtaani mpaka siyo vizuri, na kwa taarifa fupi ni kwamba ni watu wake na Baba yake na Fatuma ndo wanao kusaka na sielewi tatizo nini, yaani ukikamatwa haaa umekwisha " Mama Zena aliingia na kuanza kumsimulia Henry.


"Mama Mimi nishaamua Henry hapa nyumbani aondoke simtaki tena " 


"Zena unasemaje!? Kwa hiyo unataka Henry aende wapi!??"


"Mama atajua anako enda kwani Henry ndugu yetu!!?"


"Zena wewe asubuhi si ndo umetoka kuniambia kwamba una ujauzito wa Henry au Siyo wewe!??"


"Mama ujauzito ntalea ndiyo ila simtaki hapa nyumbani "


"Okay Henry usijali kesho naenda kukutafutia sehemu ya kukaa sawa Baba!!" Mama Zena aliona Sasa ndo Muda wa kujimilikisha Henry kwa Mara nyingine tena.


Upande wa Pili huku nyumbani kwa kina Fatuma, tayari Isabella naye aligundulika ana ujauzito na aliye gundua alikuwa ni Fatuma.


"Isabella usitake kuniambia na wewe huo ujauzito ni wa Henry!!?" Basi Fatuma ilibidi ambane Isabella.


"Aaaaaa!!! aaaaa!! Hapana siyo wa Henry!??" Isabella ilibidi Sasa akwepe tu, ila ukweli ujauzito ulikuwa wa Henry.


"Eheeee kama hiyo mimba siyo ya Henry ni ya nani, maana sijawahi kukuona na mwanaume yeyote yule!?" Fatuma alikuwa kambana haswa.


"Aaaaa!! Fatuma ntakwambia Siku nyingine!!"


"Isabella unasemaje! Siku nyingine Siku ipi!?? Ebu nambie Saiz nijue nakusaidia vipi maana Baba akijua utafukuzwa kama mbwa hapa nyumbani" Fatuma alianza kuongea kwa ukali.


"Heeeee Fatuma kuna nini Mbona unamkoromea mwenzio!" Muda huo huo Mama Filomena naye alifika alikuta Fatuma kambana Isabella na maswali.


"Mama!, Isabella ana mimba, Labda muulize wewe ni mimba ya nani!, Maana nina wasiwasi isije ikawa ya Henry!!"


"Heeeee!! Isabella una mimba na wewe!? Hii nyumba imepatwa na balaaa gani Jamani!?? Isabella Mimi sitaki kujua mimba ni ya nani ila naomba kabebe mabegi yako uondoke, na sidhani Kwa hili kama Baba Filomena atakutetea tena" Mama Filomena alipata Sasa Sababu ya kumfukuza binti huyo, maana kila Siku alikuwa anatafuta Sababu alikuwa haipati.


"Mama samahani!! Mimi ntaenda wapi Sasa jamani!??" Isabella aliongea kwa kujitirisha huruma.


"Utaenda wapi!!, nenda kwa huyo huyo aliye kupatia ujauzito unamuuliza nani Sasa!?? Fatuma ebu kamtolee mabegi yake aondoke!" Mama Filomena alikuwa kadhamiria kumtimua Filomena, na tena alitaka amatimue Kabla Mr madini hajarudi.


"Kwa hiyo unataka niende kwa aliye nipa ujauzito, we unamjua huyo aliye nipa ujauzito!??" Mama Filomena alishangaa kusikia Isabella anaongea kwa kujiamini, yaani aliacha kujitirisha huruma alianza kuongea kwa kujiamini.


"Isabella unasemaje we mpuuzi, alafu unanipandishia sauti we kama nani, ntakuwasha makofi we mpuuzi, unataka Mimi nijue aliye kupa ujauzito inanihusu!" Mama Filomena naye aliongea kwa ukali.


"Hata kama haikuhusu hapa siondoki, na kama unataka niende kwa aliye nipatia huu ujauzito ndo nimekuja hapa Sasa, kwa Sababu huu ujauzito ni wa mumeo Mr madini, kwa hiyo Sina pa kwenda" Isabella aliongea maneno ambayo yalifanya Mama Filomena na Fatuma wote wachoke, yaani Mama Filomena Sura ilimshuka kama kanyeshewa na mvua.


"Heeeee!! Isabella una!! una!! Unataka uniambie wewe ulikuwa unatembea na mume Wangu!??" Mama Filomena maneno yakiwa hayamtoki vyema, aliuliza huku midomo ikiwa inatetemeka.


"Hilo siyo swali ni Jibu na kama unataka kujua maelezo kamuulize mumeo!" Isabella alijibu kwa nyodo bila hata wasiwasi.


"Inamaana ndo maana Baba Filomena kila Muda alikuwa anakutetea wewe kufukuzwa hapa ndani, Isabella nasemaje nakuua wewe mwana hidhaya!" Mama Filomena alijikuta anapatwa na hasira za ajabu.


Muda huo huo wapo pale sebuleni wakiwa na taharuki kubwa huku wanabishana Mara Mr madini naye aliingia akiwa anajiongelesha pekee yake kwa hasira, maana ni Siku nyingine walikuwa wamemkosa Henry huko mtaani.


Je upi mwisho wa Henry!? tukutane sehemu ya mwisho ya Hadithi hii kujua Hatima ya yote

GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO (25)


.

Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group