MAAJABU YA MGENI SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA (21)


 Sehemu 21 🔞


"Henry leo sikuachi Baba Yangu, liwalo na liwe haiwezekani unanikalia kimya kwenye Simu, siwezi Henry" Filomena alifika bila hata Salam alianza kulalamika.


"Daaaaa!! Filomena Mimi siwezi tena kuwa na wewe jamani, kwa nini usitafute tu Mtu mwingine!??"


"Henry siwezi nasema siwezi, Henry wewe ndo ulinifundisha mapenzi, alafu eti kiwepesi tu nikuache, haki ya Mungu Henry sikuachi leo!!"


"Duuuu! Hii shida Sasa! Eheeee haya Sasa wewe unatakaje maana Mimi nimekuja kazini alafu unasema huniachi we unatakaje" 


"Henry kama vipi naomba tutafute sehemu basi tukaongee vizuri, maana mwenzako siyo kumiss huko" Filomena aliongea maneno ambayo yalifanya Henry acheke, maana Henry alijua kitu anacho kimanisha Binti huyo.


"Eeeeee!! Hivi Filomena hamuwezi waza mambo mengine, yaani nyie Muda wote tu munawaza ngono jamani wanaume si wapo wengi, yaani asubuhi subuhi Saiz unasema umenimiss, aaaaaa Filomena niache basi jamani" Henry aliongea kama utani ila ndo alikuwa anamanisha.


"Henry kiukweli Leo Mimi kukuacha ni mpaka unitimizie haja Zangu, siwezi na Kazi sidhani kama utafanya leo, yaani ni Bora nikose Vipindi chuo"Filomena aliongea akiwa siliasi.


"Okay Filomena katafute sehemu iliyo tulia, ukishapata njoo unichukue, ila ni lisaa limoja tu" Henry ilibidi akubali kishingo upande ilimladi tu kuondoa kero.

Basi Filomena kusikia vile alifurahi kweli kweli dakika zile zile alitoka na kwenda kutafuta lodge iliyo tulia.


Huku kwa Fatuma nako baada ya kuona hamuoni Filomena asubuhi asubuhi pale nyumbani, akili yake ilimtuma Moja kwa moja kwamba huwenda kaelekea kwa Henry.

Fatuma wivu ukiwa umemjaa alijiandaa haraka haraka na kuchukua Gari kisha alitoka, safari yake ilimpeleka Moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Henry anako kaa.


Ila baada ya kufika pale kitu Cha maajabu Fatuma alimkuta Isabella akiwa anachungulia chungulia getini, yaani kama mwizi hivi.


"Eheeee Isabella kilicho kuleta huku nini na aliye Kuonesha huku nani!??" Isabella akiwa anachungulia alishitushwa na Sauti ya Fatuma nusura akimbie.


"Duuuu!! Fatuma umenishitua mpaka siyo vizuri eti!!"


"Isabella nipo siliasi ujue, nakuuliza unafanya nini huku!??"


"Heeeee jamani Mimi namtafuta Henry kwani vipi!?"


"Isabella yaani asubuhi subuhi umeacha Kazi kule nyumbani umekuja huku, au umechoka Kazi eee, alafu Isabella naona Siku hizi umeanza kusahau kama wewe ni mfanyakazi pale nyumbani yaani unajiamulia tu siyo"


"Aaaaa!! Fatuma unacho fanya wewe fanya tu, Mimi napigania penzi langu kwa Henry!" 


"We mpuuzi kweli!! Kisingekuwa kidomo domo chako we unafikri Henry angekimbia pale nyumbani "


"Bwana eeee!! Hayo Mimi sijui ila ninacho jua ni kwamba Mimi ndo nilikuwa wa kwanza kuwa na Henry basi!" 

Mabishano ya Isabella na Fatuma yalikuwa makali muno pale getini kwa watu, mpaka Fatuma aliona ni upuuzi aliamua kuondoka kuelekea chuo.


Fatuma kufika tu chuo Zena alimdaka juu juu, na Siku zote Zena alikuwa ni binti asiye na aibu yaani yeye alikuwa hajui kuvunga.


"Hahaaaa!! Fatuma ndo maana mnang'ang'ania yule mkaka namna hiyo wewe na Mama Yangu, kumbe yule kaka anajua vile, nakwambia Mwaka huu tutabanana mpaka mwisho, maana siyo kwa mechi ile shoga Yangu " Zena alimpasha maneno ya uchungu muno Fatuma, yaani Fatuma alipata hasira nusura ya kupasuka.


"Zena we mnafiki mjinga mmoja wewe, Mtu na akili zako hovyo, yaani Mama yako na wewe munaona ni akili kulala na mwanaume mmoja!?"


"Hahaaaa hilo mi halinihusu shoga, na kwa taarifa yako Mama kahonga mpaka Duka, kwa hiyo usitarajie huyo bwana ako kama ataachana na Mama Yangu ni leo"


"Unasemaje Zena!! Mama yako kampa Henry Duka!??"


"Unashanga nini Sasa!?? Kama huamini nenda kwenye duka letu la pale kona kama hutomkuta bwana yako kakalia kiti Cha uboss" Zena alitoboa Siri ya wapi Henry anapatikana.

Fatuma baada ya kupewa taarifa hiyo alipandwa na wazimu, yaani alitoka nduki kuelekea huko duka lilipo, maana duka hilo la kina Zena alikuwa analijua vizuri.


Dakika kumi nyingi, Fatuma alifika pale dukani baada ya kuulizia Fatuma alipewa maelezo kwamba Henry katoka Mara Moja na Dada mmoja hivi, kwa maelezo aliyo pewa Fatuma moja kwa moja alijua ni Filomena.


"Filomena mpuuzi sana! Ananifanyia Mimi hivi, sasa we subiri Moto utachimbika hii leo, nasema simuachi Mtu kama ni undugu na ufe tu" Fatuma akiwa nje ya Duka lile alikuwa anajisemea maneno kwa hasira tena alikuwa anajiongelesha kwa sauti kabisa.

Dakika zile zile Fatuma yupo pale alimuona Henry na Filomena wanashuka kwenye bajaji kwa pamoja na wanakuja pale dukani.


"Heeeee!!! Henry Fatuma yule! Mimi naondoka tutawasiliana basi" Filomena baada ya kumuona Fatuma ilibidi ageuze na aliisimamisha Bajaji na kupanda kuelekea nyumbani.


"Henry!! Ndo nini hivyo nakuuliza Henry ndo nini hivyo kuniachanganya Mimi na ndugu Yangu!? Henry tatizo kupendwa au tatizo nini, yaani unajiona unajua sana mapenzi unahisi una haki ya kufanya unacho jisikia, Henry nasema umenikosea Sana, Bora ungesema tangia mwanzo siyo kwa hiki unacho kifanya, yaani wanawake wote hujaona mpaka ndugu Yangu!??" Fatuma akiwa anamwaga chozi aliongea kwa machungu kweli kweli mpaka Henry alijikuta anakosa Cha kujibu.


Dakika zile zile Mama Zena alitia Timu na Gari yake pale dukani.


"Heeeee!! Henry nini tena kinaendelea hapa, mbona sielewi!?" Baada ya Mama Zena kufika alishuka kwenye Gari na kuuliza kwa jaziba.


"Aaaaa!! Ni huyu tu kaja hapa kunisumbua si unajua tena" Henry alijitetea ili kulinda ulaji, maana Mama Zena ndo alikuwa anamuweka mjini.


"Pumbavu unasemaje Henry, nakusumbua, yaani kukwambia ukweli unasema nakusumbua, Mama Zena huyu Henry ni mjinga asiye na akili na sijui wewe ndo umemfundisha ujinga, haiwezekani aniachanganye Mimi na ndugu Yangu, alafu Mama Zena kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui Henry kalala na Zena tena mpaka Saizi wana mahusiano, kwa hiyo usijione mshindi Sana." Fatuma aliamua kuharibu mambo, maana aliona Sasa Henry ni kama ashaanza kujiona ni mwamba.


"Eeeeee!! Mbona sielewi haya mambo Henry anacho ongea Fatuma ni kweli au!?" Mama Zena akiwa kaanza kupaniki aliuliza.


"Aaaaa!! Hapana Muongo, wivu tu huo ndo unamsumbua dear hakuna kitu kama hicho!!" Henry akiwa anababaika alijibu huku kijasho kikiwa kinamtoka.


"Unasemaje Henry wivu!! Muda huu umetoka wapi!?! Wewe hujatoka kufanya uchafu na Filomena!? Nakuuliza umetoka wapi na ndugu Yangu!!?haya wewe majuzi juzi hujalala na Zena!? tena Zena mwenyewe kwa mdomo wake kaniambia kila kitu, eheee upi uongo hapo!? We mwanaume Malaya sijawahi ona au unajivunia kisa unasifiwa kwamba unajua mapenzi, mpuuzi mmoja wewe na Henry nakwambia Mwaka huu ntakufanyia balaa huu mji utauona mchungu " Fatuma alikuwa kavurugwa kupita kiasi, yaani kitendo Cha Henry kulala na Filomena alafu na yeye kilimuuma muno aliona kama ni udhalilishaji Fulani hivi, sijui Fatuma angejua kama Henry amewahi lala na Mama yake ingekuwaje.


Baada ya Mama Zena kuambiwa maneno yale hapo alikumbuka Jana yake Jinsi Henry na Zena walivyo kaaa Muda mrefu bila kuonekana pale dukani, alafu baada ya kurudi Henry akatoa Sababu zisizo eleweka, hapo Mama Zena aliona kijana Henry ni kama Sasa kaanza dharau.


"Henry hivi wewe unanionaje kwanza Mimi!? Unaniona kama punguani eeee!?? Pumbavu zako wewe ndo wakunichanganya Mimi na binti Yangu, na inaonekana wewe ni tabia yako kula kuku na mayai, Sasa Henry nakwambiaje kila kitu Changu nilicho kupa utakitapika mpuuzi mmoja wewe, au unafikri wewe mwanaume Sana!??" Mama Zena alijikuta hasira zinampanda pale pale, kwanza ilibidi aende akawaulize Vijana wa mule dukani kama Henry alikuwepo kwa muda huo, baada ya kupewa maelezo yote hapo alithibitisha kwamba Henry ni kweli katoka kuzagamuana na mwanamke mwingine.


Kwa hasira Mama Zena alimchukua Henry na kuondoka naye pale dukani, walienda mpaka nyumbani na Muda huo Isabella naye alikuwa bado anazuga zuga Mitaa ile kusubiri mpaka amuone Henry.

Isabella akiwa kakaa sehemu aliona gari inafika pale na kuzama getini, basi Isabella alikimbilia getini kwenda kuchungulia nini kinaendelea, Isabella aliona Henry akiwa kashikwa Mkono na Mama Zena huku akiwa hasikii maneno yanayo zungumzwa.


"Henry naomba uchukue kila kilicho chako uondoke, mwanaume gani hufadhiliki, kosa langu lipi kukupenda au!?  Yaani wewe unataka unichanganye Mimi na Mwanangu kama ulivyo fanya kwa Fatuma na Mama yake, na sidhani Fatuma akijua kama wewe unatembea na Mama yake kama atakuacha "


"Dear!! Please nisamehe sirudii tena ni shetani tu alinipitia " Henry alikuwa anabembeleza mpaka siyo vizuri.


"Henry ebu toka, kwanza nimekumbuka unavyo kuja hapa ndani hukuja na kitu chochote ebu toka kwangu, pumbavu zako kwanza na hiyo Simu lete maana nayo nimekununulia Mimi " Mama Zena alikuwa na hasira isiyo na kipimo.


"Mama Zena basi nitolee laini, maana kwenye laini kuna pesa Zangu ujue "


"Pumbavu hupati kitu, bora usingeniambia kama pesa umeweka kwenye laini, kwanza laini zenyewe si nilikusajilia mwenyewe, Sasa wewe toka na kwa taarifa yako naenda kumpatia taarifa Mr madini kuhusu wewe na mkewe uona kama hujaenda kunyea Debe." Mama Zena alikuwa anaongea mpaka mate yanamtoka.


Basi Mama yule alimtimua Henry pale ndani kwa nguvu, na Henry hakutoka hata na shilingi mia kwa Sababu pesa zake zote Henry alikuwa anatunza kwenye laini.

Isabella akiwa katulia sehemu aliona getini Henry na Mama Zena wanasukumana, Henry alikuwa anaomba asifukuzwe Mama Zena alikuwa hamtaki.


Baada ya Mama Zena kufanikiwa kumtoa Henry mpaka nje alifunga geti na dakika hiyo hiyo alimpigia mwenye nyumba kwamba aje amkabidhi nyumba yake, maana alikuwa hayupo tayari kuendelea kukaa tena pale.


Je ndo mwisho wa Henry au ndo ukisema Cha nini kuna Mtu mwingine anasubiri pembeni!???


Itaendelea......... 


Usikose sehemu ya 22

GUSA HAPA KUSOMA SEHEMU YA ISHIRIRNI NA MBILI (22)


Chapisha Maoni

Join Our
Whatsapp Group