SEHEMU YA 18
*
Sikuridhika, ilipofika siku ya jumamosi, nilichukua gari yangu makusudi nikasema ngoja niende kigamboni pale kwake nikamuona huenda akanieleza labda nilikosea wapi, nilipofika kigamboni nilipaki gari nje ya geti halafu nikagonga, nilipogonga alifungua yule kijana ambaye alikuwa anaishi pale mara zote.
“Mambo” nilimsalimia
“Safi kwema?” aliniuliza yule aliyefungua geti
“Kwema, samahani namkuta Rayan?” niliuliza
“Rayan?” aliniuliza
“Yes”
“Hapana”
Ghafla nikasikia sauti ndani, “Oya nani huyo?” aliuliza mtu aliyekuwa ndani
“Sister mmoja hivi” alisema yule kijana
“Mwambie aingie” alisema yule mtu
“Karibu sister” yule mfungua geti aliniambia
“Asante” niliingia ndani ya geti, na nilipotazama nilimuona yule rafiki yake Rayan ambaye alikuwa na rasta, akiwa anavuta sigara kwenye kiti cha plastic nje ya nyumba yake.
Nikamuuliza “Habari shem” maana nilikuwa namfahamu hata siku ile ya birthday yangu alikuwepo mlimani city na wote walinipa zawadi.
“Ah kumbe shemeji, karibu bwana aah” alisema rasi kwa furaha huku akiinuka na kuniambia “Njoo ukae”
“Asante sana shemeji, ila sikai sana, nilikuwa naomba kuongea na Rayan” nilisema
“Rayan?” aliniuliza
“Ndio…Rayan maana kila nikimpigia simu kaniblock, yaani hata WhatsApp kaniblock”
“Ndo ukae sasa nikueleze”
“Daaah jamani” nilisema huku nikisogea nikakae kwenye kiti
“Kwani Rayan alikuambia anakaa hapa?”
“Ndio, nilikuja naye tukakaa sana hapa, akaniambia ni kwake kwa hiyo nilikuwa naomba kama inawezekana niweze kukutana naye anieleze wapi nimemkosea”
“Aaaah dada yangu si una mchumba wewe?” aliniuliza nikashtuka
“Sijakuelewa kaka, una maana gani?”
“Namaanisha kwamba si ulisema una mchumba mwingine nje na Rayan?”
“Ndio, lakini……”
“Ah ah, achana na maneno mengi, acha nikushauri tu kitu kimoja, achana na Rayan”
“Unamaanisha nini shem?”
“Yule tapeli tu hapa mjini, nafikiri siku mmeenda kumkamata mlifika kwake”
“Ndio lakini aliniambia pale ni pa kuzugia tu”
“Sasa pale ndio kwake, sisi ndio tunamuweka town, yule atakupotezea muda wewe komaa na mchumba wako”
“Ina maana hapa sio kwake kama alivyosema?”
“kwani alikuambia hapa ni kwake?”
“Ndio”
“Ah, alikutapeli tu uingie kingi, mi nikushauri kitu kimoja, yule achana naye, mi si ni msela wangu namjua vizuri….wewe unaonekana una future achana na watu wa ajabu” alinipa onyo
Nilishangaa kabisa, sikuamini Rayan ni tapeli kiasi kile, nikaona ni heri basi nikaachana naye kweli, nikafuata mambo yangu,
Nilimuaga rafiki yake na kuondoka zangu. Nilipofika nyumbani nilijicheka na kusema kimoyo moyo “Yule mwanzoni nilijua ni mlaghai halafu kaja kunilaghai..ama kweli wanawake sisi”
Niliamua kujituliza kwenye penzi langu na Meshack, sikutaka kushawishiwa na mtu yeyote suala zima la mahusiano, nilikuwa sitaki mwanaume mwingine tena maana nilihisi wote ni matapeli
Kweli sikumtafuta Rayan wala yeye hakunitafuta tena
MWISHOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
